Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Philipo Gekul.

Pia, soma: Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

F_yxrssW0AArgGd (1).jpeg

Saa chache zilizopita, Pauline Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini alituhumiwa kumfanyia unyanyasaji mfanyakazi wake ambapo inadaiwa akishirikiana na watu wengine walimdhuru mwili na kumuingiza chupa sehemu ya haja kubwa.

Hata hivyo, Mbunge Pauline kupitia Katibu wake alikanusha taarifa hiyo katika ujumbe uliowekwa kwenye mitandao ya kijamii ukimtuhumu Hashimu kufanya udanganyifu na kushirikiana na washindani wa Pauline wa kibiashara kumfanyia ushirikina na baadaye ujumbe huo kufutwa kwa maelezo kuwa suala hilo liko mikononi mwa Polisi.

Pia soma: Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto
 
Maoni ya juzi ya mh. Jakaya Kikwete na leo hii ya Jenerali Ulimwengu n.k kuwa rais akubali maoni ya wananchi kwa vile ni ngumu sana rais kufahamu kila kinachotendeka katika nchi hii kubwa yenye eneo la kilometa za mraba zaidi ya 900,000.
Kikwete - Rais uwe msikivu maoni ya wananchi
View: https://m.youtube.com/watch?v=hp8zwwtz-Go


Picha kutoka maktaba :

Naibu waziri wa Katiba na Sheria, Mh. Pauline Gekul akichangia makadiroo ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria mwaka 2023/2024 Jumanne Aprili 25,2023.


View: https://m.youtube.com/watch?v=q4T8rdTdGIk
Mbunge - Pauline Philipo Gekul
Naibu Waziri - Wizara ya Katiba na Sheria
Eneo bunge Jimbo - Babati Mjini
Chama cha siasa : CCM
Elimu - Masters UDOM 2014
Elimu - Degree ya kwanza UDSM 2006
 
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Philipo Gekul.

View attachment 2824966
Safi, Hapa namkubali Samia, Ingekuwa kipindi cha yule egomaniac psychopath angempndisha cheo na kumfanya waziri kamili, huku akijivunia kuwa SIPANGIWI
 
Back
Top Bottom