Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Philipo Gekul.

View attachment 2824966

Saa chache zilizopita, Pauline Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini alituhumiwa kumfanyia unyanyasaji mfanyakazi wake ambapo inadaiwa akishirikiana na watu wengine walimdhuru mwili na kumuingiza chupa sehemu ya haja kubwa.

Zaidi soma,

Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili Mtoto

Usaliti ni laana
 
Nilifikiri angeanza kuwasimamisha wale wahujumu uchumi waliotajwa kwenye ripoti ya CAG, nk. Kabla ya kuanza na huyu aliyeshutumiwa. Maana bado ukweli halisi haujajulikana!

Au alikuwa anamvutia kasi ili nafasi yake ichukuliwe na mwingine?
Nenda na wewe ukakalie chupa kama imekuuma huyu boss wako kutenguliwa
 
Huyo Waziri angeshauriwa ajiuzulu kwa maslahi ya chama na serikali.

Kitendo cha kutenguliwa kinatengeneza mfano mbaya kwa watendaji wa serikali.

Tutashuhudia clip nyingi sana za maovu ya viongozi kwa wananchi, na wasipotenguliwa ndio shughuli itaanzia hapo.
 
Back
Top Bottom