Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Philipo Gekul.

View attachment 2824966

Saa chache zilizopita, Pauline Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini alituhumiwa kumfanyia unyanyasaji mfanyakazi wake ambapo inadaiwa akishirikiana na watu wengine walimdhuru mwili na kumuingiza chupa sehemu ya haja kubwa.

Zaidi soma,

Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili Mtoto

Mama una kura yangu
 
Maoni ya juzi ya mh. Jakaya Kikwete na leo hii ya Jenerali Ulimwengu n.k kuwa rais akubali maoni ya wananchi kwa vile ni ngumu sana rais kufahamu kila kinachotendeka katika nchi hii kubwa yenye eneo la kilometa za mraba zaidi ya 900,000.

Picha kutoka maktaba :

Naibu waziri wa Katiba na Sheria, Mh. Pauline Gekul akichangia makadiroo ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria mwaka 2023/2024 Jumanne Aprili 25,2023.

View: https://m.youtube.com/watch?v=q4T8rdTdGIk
Mbunge - Pauline Philipo Gekul
Naibu Waziri - Wizara ya Katiba na Sheria
Eneo bunge Jimbo - Babati Mjini
Chama cha siasa : CCM
Elimu - Masters UDOM 2014
Elimu - Degree ya kwanza UDSM 2006

Hakuwa chadema huyu? Ni swali tu
 
Kwamba huyo Pauline aliamuru kijana awekewe chupa matakoni? Kwamba huyo Gekul nae ni muumini wa ufiraji na ukatili, yaani katika adhabu zote akaona hiyo ndio inafaa kijana kupewa? Iwe tuhuma au kweli, hatakiwi kuwa waziri na hapa ndipo katiba inatakiwa kuangaliwa tena, hafai hata huo ubunge. Nasema iwe tuhuma au iwe imethibitika.
Naungana na wew ila kusema hata kwa tuhuma tu mtu hafai kuwa mbunge huo sasa utakuwa wendawazimu, leo watu wakizusha tuhuma juu ya Mbowe nae itabidi ajiuzulu bila kuthibitisha?
 
Huyu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Philipo Gekul.

View attachment 2824966

Saa chache zilizopita, Pauline Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini alituhumiwa kumfanyia unyanyasaji mfanyakazi wake ambapo inadaiwa akishirikiana na watu wengine walimdhuru mwili na kumuingiza chupa sehemu ya haja kubwa.

Zaidi soma,

Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili Mtoto

Huyu apandishwe kizimbani
 
Back
Top Bottom