Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Haki za watoto
1. Watoto wamecheza Honey, mwalimu mkuu alitumbuliwa
2. Huyu kamuingiza chupa na kumpiga mtoto tuone atabaki na ubunge wake?
Hapa tutaona Double Standards
Waziri wa watoto upo?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Philipo Gekul.

View attachment 2824966

Saa chache zilizopita, Pauline Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini alituhumiwa kumfanyia unyanyasaji mfanyakazi wake ambapo inadaiwa akishirikiana na watu wengine walimdhuru mwili na kumuingiza chupa sehemu ya haja kubwa.


Hata hivyo, Mbunge Pauline kupitia Katibu wake alikanusha taarifa hiyo katika ujumbe uliowekwa kwenye mitandao ya kijamii ukimtuhumu Hashimu kufanya udanganyifu na kushirikiana na washindani wa Pauline wa kibiashara kumfanyia ushirikina na baadaye ujumbe huo kufutwa kwa maelezo kuwa suala hilo liko mikononi mwa Polisi.

Mama msikivu kasikia maoni ya Great thinkers Jana tulikuwa moto balaaa
 
Haki za watoto
1. Watoto wamecheza Honey, mwalimu mkuu alitumbuliwa
2. Huyu kamuingiza chupa na kumpiga mtoto tuone atabaki na ubunge wake?
Hapa tutaona Double Standards
Waziri wa watoto upo?

Waalimu wakuu hawakutumbuliwa Bali walivuliwa cheo Cha ualimu mkuu, ila kwa Sasa wamerejeshewa ualimu mkuu maana hawakuwepo shuleni kipindi jambo Hilo linatokea.
 
Mkuu bado ni tuhuma tu, usihukumu, mamlaka pekee ya kuhukumu ni mahakama!
Yawezekana, lakini ukisoma maelezo ya waziri kupitia Katibu wake, na ukosoma yale ya kijana hata bila kuwajua wote wawili, utagundua kuna mmoja kati yao analinda status yake
 
Maoni ya juzi ya mh. Jakaya Kikwete na leo hii ya Jenerali Ulimwengu n.k kuwa rais akubali maoni ya wananchi kwa vile ni ngumu sana rais kufahamu kila kinachotendeka katika nchi hii kubwa yenye eneo la kilometa za mraba zaidi ya 900,000.


Picha kutoka maktaba :

Naibu waziri wa Katiba na Sheria, Mh. Pauline Gekul akichangia makadiroo ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria mwaka 2023/2024 Jumanne Aprili 25,2023.


View: https://m.youtube.com/watch?v=q4T8rdTdGIk
Mbunge - Pauline Philipo Gekul
Naibu Waziri - Wizara ya Katiba na Sheria
Eneo bunge Jimbo - Babati Mjini
Chama cha siasa : CCM
Elimu - Masters UDOM 2014
Elimu - Degree ya kwanza UDSM 2006

 
Back
Top Bottom