Rais Samia ateua na Kutengua Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA)

Rais Samia ateua na Kutengua Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kama ifuatavyo:

i) Amemteua Bw. Frank Kanyusi Frank kuwa Kabidhi Wasii Mkuu. Kabla ya uteuzi Bw. Frank alikuwa Mwanasheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Bw. Frank anachukua nafasi ya Bi. Angela Kemanzi Anatory ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

ii) Amemteua Bi. Irene Joseph Lesulie kuwa Naibu Kabidhi Wasii Mkuu. Kabla ya uteuzi Bi. Lesulie alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mashauri ya Kimataifa, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Bi. Irene anachukua nafasi ya Bi. Lina Robert Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Uteuzi huu umeanza tarehe 08 Juni, 2023.

View attachment 2653875
Wagalatia uwezi kuwaona hapa, na waislam huwezi kuwasikia wakilalama
 
..waliotenguliwa wataendelea kulipwa MISHAHARA bila kufanya kazi.
 
Angela hakuaharibu kazi amejitahidi sana kuitengeneza Rita na kuzuia upigaji ila Naibu wake ndo amemuangusha
Dah, Mungu atamuinua zaidi:
RITA kuna upigaji kuliko hata TRA na BANDARI.
RITA upande wa usajili wa TRUST pale kwa wanasheria na bosi wao, RITA upande ambao wanapewa wawe wasimamizi wa MIRATHI yenye ugomvi aisee ni shamba la bibi, tatizo wanao umizwa hawana pa kwenda maana ile ni SERIKALI.

#hongera MAMA SAMIA, kwa kutupia jicho RITA

##MAMA SAMIA ikumbuke BRELA, upigaji wake upo sawa au level moja na TRA.
BRELA wanatumia mamilioni kuzunguka nchi nzima semina zisizo na maana na kulipaana mamilioni ya posho, waziri amekaa kimya, wafanyakazi wanajizolea mafedha tu bila huruma.
 
Kwenye vyeti vya kuzaliwa sasa kutakuwa na jina la Kanyusi. Dada Anatory kakosea nini?Au kawapa vyeti vya kuzaliwa wakimbizi?
Pengine huko mitaani amesikika akilaani makubaliano yale ya kishenzi ya kuwapa bandari yetu DP kwa mkataba wa milele.
 
Back
Top Bottom