Rais Samia atishwa na kasi ya ongezeko la Idadi ya Watu, lisilioendana na kasi ya ukuaji wa Uchumi wetu

Rais Samia atishwa na kasi ya ongezeko la Idadi ya Watu, lisilioendana na kasi ya ukuaji wa Uchumi wetu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rais Samia, ameonya juu ya ongezeko la idadi ya watu lisiloendana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

Akizungumza leo, Februari 1, 2025, katika uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, toleo la 2023, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Mrisho Kikwete, jijini Dodoma, Rais Samia amesema kuwa kwa ukuaji wa asilimia 3.2% kwa mwaka, idadi ya watu nchini inakadiriwa kufikia milioni 123 ifikapo mwaka 2044.

"Ongezeko la Idadi ya Watu, lisilioendana na kasi ya ukuaji wa Uchumi wetu. Kwa ukuaji wa asilimia 3.2% kwa mwaka, inakadiriwa kwamba ifikapoa 2044 idadi ya watu hapa nchini itakuwa milioni 123 na hivyo kuongeza mahitaji ya kazi na ajira"

Soma, Pia:
Rais Samia anazindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo La 2023, Dodoma

 
Kwa hili wafahidhina wa dini na conspiracies watampinga sana
 
Na hapo hajaambiwa bajeti ya wahitaji chanjo, condom, vyandarua na ARV baada ya Trump kufunga fuko lililokuwa linagharimia huduma hizo
 
Yani form one wapo 500, dawati moja wanafunzi wa 3
 
Tanzania ni nchi kubwa sana, acha watu waendelee kuzaliana. Na kama nchi iwekeze kwenye vipaumbele muhimu.
Kwa hiyo unataka watu waendelee kuzaliana kama mapanya, Halafu huduma za kijamii bado ni za kusua sua?
 
Ongezeko la watu,linamaanisha ongezeko la nguvu kazi,ongezeko la ukubwa wa SOKO n.k.
Nashangaa Rais analalamika.
 
Rais Samia akizungumza leo, Februari 1, 2025, katika uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, toleo la 2023, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Mrisho Kikwete, Jijini Dodoma, amesema "ongezeko la Idadi ya Watu, lisilioendana na kasi ya ukuaji wa Uchumi wetu. Kwa ukuaji wa asilimia 3.2% kwa mwaka, inakadiriwa kwamba ifikapoa 2044 idadi ya watu hapa nchini itakuwa milioni 123 na hivyo kuongeza mahitaji ya kazi na ajira"

Soma, Pia: Rais Samia anazindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo La 2023, Dodoma

Aione Lucas Mwashambwa mezani kwake na abubujikwe machozi haraka
 
Tanzania kuna kipi ilichowekeza zaidi ya uchawa na kumsifia mama?
Hivi hapo umejibu kitu nimechouliza kweli, kama inawekeza kwenye vitu vya kijinga kwa nini usiwekeze kwenye vitu vya maana Ili ongezeko wa watu liendani na huduma bora kwa wananchi?.
 
Japan wana watu wengi kuliko tanzania na eneo lao ni dogo ila wana mipango madhubuti
Je tanzania hilo wanalo au ndiyo bora liendeeee

Ova
 
Nguvu kazi ya betting and bodaboda?
Hapo mwenye kosa lipo kwa hao bodaboda au mkusanya kodi,ambaye pesa nyingi anazipeleka kununua V8 na kufanya uchaguzi ambao matokeo yake yanajulikana na mwishowe kutoa kauli ya 'KILA MBUZI ALE KULINGANA NS UREFU WA KAMBA YAKE?'
 
Hivi hapo umejibu kitu nimechouliza kweli, kama inawekeza kwenye vitu vya kijinga kwa nini usiwekeze kwenye vitu vya maana Ili ongezeko wa watu liendani na huduma bora kwa wananchi?.
Ulisema watu waendelee kuzaliana, Sasa nikakuuliza, Unataka watu waendelee kuzaliana kwa huduma zipi za kuwatosheleza?
 
Back
Top Bottom