Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Katika kuboresha huduma za mifugo na kuiepusha dhidi ya magonjwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia matumizi ya jumla ya Shilingi Bilioni 5.9 kwa ajili ya ujenzi wa majosho 257 katika Halmashauri 80, ambapo kati ya hayo tayari majosho 88 yamekamilika.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (Mb) amebainisha hayo katika Kijiji cha Narakauo kilichopo Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakati akihitimisha ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kukagua miradi ya ujenzi wa mabwawa kwa ajili ya mifugo, huku akibainisha majosho ambayo yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi ni 169.
Akizungumza na jamii ya wafugaji Mhe. Ulega amesema katika kuhakikisha lengo na dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuokoa afya ya mifugo ya wafugaji katika mwaka wa fedha 2022/23, vifo vya mifugo vinavyotokana na maradhi ya kupe na ndorobo vimepungua kutoka asilimia 72 hadi 56.
Ameongeza kuwa tayari majosho matano yamejengwa katika Wilaya ya Simanjiro mwaka huu wa fedha, majosho mawili mwaka uliopita na majosho saba yatajengwa mwaka ujao wa fedha.
Aidha, amesema licha ya ujenzi wa majosho serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa dawa ya ruzuku kwa ajili ya kuweka kwenye majosho lita 52,560 kote nchini zenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.3, huku takriban lita 400 zikipelekwa katika Wilaya ya Simanjiro kwa ajili kuzitawanya katika majosho yaliyopo kwenye wilaya hiyo.