Rais Samia atoa bilioni 5.9 kuboresha afya ya mifugo

Katika kuboresha huduma za mifugo na kuiepusha dhidi ya magonjwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia matumizi ya jumla ya Shilingi Bilioni 5.9 kwa ajili ya ujenzi wa majosho 257 katika Halmashauri 80, ambapo kati ya hayo tayari majosho 88 yamekamilika.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (Mb) amebainisha hayo katika Kijiji cha Narakauo kilichopo Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakati akihitimisha ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kukagua miradi ya ujenzi wa mabwawa kwa ajili ya mifugo, huku akibainisha majosho ambayo yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi ni 169.

Akizungumza na jamii ya wafugaji Mhe. Ulega amesema katika kuhakikisha lengo na dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuokoa afya ya mifugo ya wafugaji katika mwaka wa fedha 2022/23, vifo vya mifugo vinavyotokana na maradhi ya kupe na ndorobo vimepungua kutoka asilimia 72 hadi 56.

Ameongeza kuwa tayari majosho matano yamejengwa katika Wilaya ya Simanjiro mwaka huu wa fedha, majosho mawili mwaka uliopita na majosho saba yatajengwa mwaka ujao wa fedha.

Aidha, amesema licha ya ujenzi wa majosho serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa dawa ya ruzuku kwa ajili ya kuweka kwenye majosho lita 52,560 kote nchini zenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.3, huku takriban lita 400 zikipelekwa katika Wilaya ya Simanjiro kwa ajili kuzitawanya katika majosho yaliyopo kwenye wilaya hiyo.

View attachment 2524982
Nimemsikia mama akiwasisitizia viongozi kuwa Urais ni taasisi, sasa iweje kila siku tunaambia kuwa katoa mabillioni kufanya hiki na kile, badala ya kutuambia kuwa serikali imetoa hela kutekeleza miradi hii?
Wote tunafahamu kuwa Rais hana hela na hajawahi kuwa na hela tofauti na HH wa Zambia. Mshahara wake tunaufahamu.
 
Kwani anayetoa ni nani?
 
Kwahiyo hela anatoa mfukoni mwake au ni hela za umma ?
Jamaa wanakosea sana kutupa taarifa hawa. Pesa inatoka kwenye kodi zetu eti wenyewe wanasema Samia katoa!!??
Kanakwamba tunaomba ama tumepewa bure kumbe ni haki na raisi anachofanya ni kutekeleza majukumu yake
 
Tengeni na maeneo ya malisho ya Mifugo, kuondoa kero ya migongano kati ya mkulima na mfugaji...msiishie hapo tu, ndani ya eneo la marisho kuwepo na huduma ya visima vya maji kwaajil ya Mifugo..
Yatengwe mashamba KWAAJILI ya kupanda mbegu Bora za malisho..

Wizara ya Mifugo ni kama Wizara yatima, Huwa inasahaulika sana.
Ukiangalia chat ya nchi zenye idadi nyingi ya Mifugo kwa Afrika, sisi tupo kwenye 3 Bora..
Lakini angalia wizara isivyopewa thamani.

Mifugo hithaminiwi ila wanathamini nyama ikiwa kwenye bakuli,madafakeni yani wafugaji wa nchi hii wanateseka sana.
 
Katika kuboresha huduma za mifugo na kuiepusha dhidi ya magonjwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia matumizi ya jumla ya Shilingi Bilioni 5.9 kwa ajili ya ujenzi wa majosho 257 katika Halmashauri 80, ambapo kati ya hayo tayari majosho 88 yamekamilika.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (Mb) amebainisha hayo katika Kijiji cha Narakauo kilichopo Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakati akihitimisha ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kukagua miradi ya ujenzi wa mabwawa kwa ajili ya mifugo, huku akibainisha majosho ambayo yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi ni 169.

Akizungumza na jamii ya wafugaji Mhe. Ulega amesema katika kuhakikisha lengo na dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuokoa afya ya mifugo ya wafugaji katika mwaka wa fedha 2022/23, vifo vya mifugo vinavyotokana na maradhi ya kupe na ndorobo vimepungua kutoka asilimia 72 hadi 56.

Ameongeza kuwa tayari majosho matano yamejengwa katika Wilaya ya Simanjiro mwaka huu wa fedha, majosho mawili mwaka uliopita na majosho saba yatajengwa mwaka ujao wa fedha.

Aidha, amesema licha ya ujenzi wa majosho serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa dawa ya ruzuku kwa ajili ya kuweka kwenye majosho lita 52,560 kote nchini zenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.3, huku takriban lita 400 zikipelekwa katika Wilaya ya Simanjiro kwa ajili kuzitawanya katika majosho yaliyopo kwenye wilaya hiyo.

Watakwambia anakopa sana hawaoni kinachofanyika 🤪🤪
 
Back
Top Bottom