Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kwaniaba ya Rais Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekabidhi mitungi ya Gesi 1000, kwa Umoja wa Wajasiriamali wanaopika chakula Mkoani Arusha (Mamalishe na Babalishe), akiwasihi kuendelea kumuombea kheri kutokana na mapenzi yake makubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kama yalivyo malengo ya serikali kuwa kufikia 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, Mhe. Makonda wakati wa makabidhiano hayo, ametangaza kuwa hivi karibuni mitungi mingine 1,000 itakabidhiwa kwa wajasiriamali hao, akisema mkakati wa mkoa wa Arusha ni kuhakikisha kuwa Wajasiriamali wote wa chakula mkoani hapa wanatumia nishati safi ya kupikia kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.