Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
MIAKA 63 YA UHURU WA TANGANYIKA: Katika kuadhimisha sherehe hiyo, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan leo Disemba 09, 2024 ametoa msamaha kwa wafungwa 1548, ambapo wafungwa 22 kati yao wanaachiliwa huru tarehe 9 Disemba, 2024, na 1526 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.
Rais ametumia Mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1) (a) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa msamaha huo huku akisema ni matarajio ya Serikali kuwa wafungwa hao watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.