Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 1548

Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 1548

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
MIAKA 63 YA UHURU WA TANGANYIKA: Katika kuadhimisha sherehe hiyo, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan leo Disemba 09, 2024 ametoa msamaha kwa wafungwa 1548, ambapo wafungwa 22 kati yao wanaachiliwa huru tarehe 9 Disemba, 2024, na 1526 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.

IMG_1413.jpeg

Rais ametumia Mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1) (a) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa msamaha huo huku akisema ni matarajio ya Serikali kuwa wafungwa hao watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.

IMG_1418.jpeg
IMG_1419.jpeg
IMG_1420.jpeg
IMG_1421.jpeg
 
Orodha ya walio samehewa iwe wazi kwenye vyombo vya habari,na magereza waliko kuwa

Kuna tabia ,baada ya msamaha huu, maafisa wa magereza nao wanatoa barua zao za msamaha,kisingizio rais kawasamehe.
 
Orodha ya walio samehewa iwe wazi kwenye vyombo vya habari,na magereza waliko kuwa

Kuna tabia ,baada ya msamaha huu, maafisa wa magereza nao wanatoa barua zao za msamaha,kisingizio rais kawasamehe.
Unachana mkeka mkuu
 
Back
Top Bottom