Rais Samia atoa Nishani za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuzindua Kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nishani za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuzindua Kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika Viwanja vya Ikulu - Chamwino Dodoma tarehe 24 Aprili 2024.


View: https://www.youtube.com/live/EmRN8w3uk7w?si=SMHMMsNu_3_zvd_f

Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Salma Kikwete Nishani ya Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere aliyoipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.


Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Janeth Magufuli Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika halfa iliyofanyika lkulu Chamwino, Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.

Rais Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Samwel Malecela kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024

Rais Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tatu Mhe. Fredrick Sumaye kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein vitabu vya Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
 
Halafu wanaleta nyenyenyenye zao.
 

Attachments

  • FB_IMG_1713900678402.jpg
    43.3 KB · Views: 5
Rais wa JMT mh Dr Samia Suluhu Hassan amemtumukia Nishani ya Mwalimu Nyerere Shujaa Magufuli

Nishani hiyo kakabidhiwa mama Janeth Magufuli mjane wa Shujaa

Source: Ayo TV

Watu wa Legacy tunashangilia πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ”₯πŸ”₯
Ni kuelekea uchaguzi
 
Hongera kwake kwa kutunukiwa nishani hiyo .

Ila tukianza kuongelea yaliyofanyika enzi za "shujaa" kama kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, Leopold Lwajabe , Roma Mkatoliki, Mohamed Dewji na wengineo wengi tunaomba muwe mnazijibu hoja sio kusema aachwe apumzike wakati nishani mnampa hamuachi apumzike.
 
Tulia wewe bwege

Mbona unatumia ID feki sasa
 
Unafiki kwenye siasa ni kwa sababu ya kuwapumbaza wapumbavu tu. πŸ™ŒπŸ½ πŸ™ŒπŸ½
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa hafla ya utoaji nishani kwa viongozi mbalimbali na uzinduzi wa vitabu viwili cha Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais na safari ya picha za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni shamrashamra za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika viwanja vya Ikulu Chamwino tarehe: 24 Aprili, 2024.
 

Attachments

  • VID-20240424-WA0085.mp4
    26.1 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…