Rais Samia atoa pole ya kifo Lawrence Nyasebwa Mafuru

Rais Samia atoa pole ya kifo Lawrence Nyasebwa Mafuru

Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kilichotokea leo tarehe 09 Novemba, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.

Ninatoa pole kwa familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

Bw. Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali.


Mwenyezi Mungu aijalie familia yake subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho yake mahali pema.

Amina.

Pia Soma: TANZIA - Lawrance Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango afariki dunia
 
Back
Top Bottom