Rais Samia atoa siku 60 kwa Waajiri kulipa malimbikizo ya Bima ya Afya

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhakikisha anasimamia madai ya Bima ya Afya na tatizo la waajiri kutowasilisha michango ya Wafanyakazi.

Akizungumza kuhusu Bima ya Afya Rais Samia amemuagiza Waziri Mkuu Majaliwa kusimamia madai ya watoa huduma yanayopaswa kulipwa ndani ya siku 60 tangu kupokelewa kama inavyosema sheria ya bima ya afya sura ya 395.

"Kama mtu alijilimbikizia, ndani ya siku 60 alipe malimbikizo yote wafanyakazi wafaidike na bima zao za afya." Amesema Rais Samia

Kufuatia tatizo la waajiri kutowasilisha michango ya Wafanyakazi, Waziri Mkuu ataitisha kikao na waajiri ili kuondoa tatizo la hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…