Rais Samia atoa TZS 35BL Ujenzi wa Musoma Airport kumuenzi Baba wa Taifa

Samia naona kawa tajiri sana.

Hebu tuache hizi porojo za kusema raisi katoa kiasi fulani.

Hivi kuna ugumu gani wa kusema raisi kaidhinisha kiasi kadhaa kwaajili ya ujenzi wa kitu A
kwani hujui kuwa Samia ni taasisi?
 
Ingejengwa Butiama kama ilivyojengwa ya Chato ningeelewa. Hii airport ilihitajika siku nyingi ni uzembe tu wasituleee kumuenzi Mwalimu hapa. Kila kitu siasa WaTZ tumekosea wapi?
 
Ingejengwa Butiama kama ilivyojengwa ya Chato ningeelewa. Hii airport ilihitajika siku nyingi ni uzembe tu wasituleee kumuenzi Mwalimu hapa. Kila kitu siasa WaTZ tumekosea wapi?
Kwani Musoma iko wapi?
 
Hivi mnavyosema Samia au Magufuli katoa pesa,huwa mnamaanisha ni zao za mifukoni au ni hizi kodi zetu?
Huko nyuma sikuwahi kusikia hizi kauli za eti Kikwete au mkapa ametoa pesa kwa ajili ya mradi flani wa umma.
 
Wangeweka data za kiuchumi hapa juu ya hii Airport itaongeza nini kiuchumi kwa Musoma/Taifa sio kumuenzi Mwalimu. Hata angefufuka akasikia mmejenga musoma airport bila kuzingatia faida zilizopo kiuchumi asingefurahi. Hii Airport ilihitajika kuwa upgraded long ago na faida za kiuchumi zipo. Ila sio kumuenzi Mwalimu. Mwalimu was Saint. Msilitaje taje jina lake kwenye justification zenu za kisiasa.
 
Hivi Rais anatoa wapi pesa mpaka tuseme kwamba Rais katoa kiasi hiki na hiki kufanya mradi fulani? Are we serious?

Seriously waTanzania tunahitaji kubadilika tujitambue. Tunaona kila kinachofanywa na watawala kama tunafanyiwa hisani wakati ni kodi zetu.

Hii yote ni legacy ya mwendazake kuamini kwamba bila yeye maendeleo tutayasikia na kuyaona kwingine. Hii tabia imeanza kipindi cha Mwnedazake.

Leo katangulia kwa muumba wake..Tanzania si ipo na inaendelea kudunda?

Tubadilike. Tujiamini! Watawala watakuja na kuondoka. Tanzania itakuwepo mpaka mwisho wa dahari!

Masanja,
 
Nashangaa siasa zimebadilika na kusifia mtu badala ya wananchi. Kodi ni zetu leo imekuwa ya Rais tulimuweka sisi leo kageuka tajiri anatoa fedha mifukoni Mwake hovyo hii kabisa.
 
Nashangaa siasa zimebadilika na kusifia mtu badala ya wananchi. Kodi ni zetu leo imekuwa ya Rais tulimuweka sisi leo kageuka tajiri anatoa fedha mifukoni Mwake hovyo hii kabisa.
Kwani hujui Rais anafanya badala ya Wanachi?
 
Kwani hujui Rais anafanya badala ya Wanachi?
He/She should not take all the credits by naming him/her, better say the GOV has given the money to finance this and that and not the president. The actual allocation of funds is approved by Parliament not even the president why naming him/her, it looks as if it's a favor while it is the right of the people.
 
Hapa umebadili tu lugha
 
sikia, sote tunampenda mama, lakini ninachotajiru kukwambia ni kwamba, hizo hela hajatoa mfukoni mwake, hana hela kama hizo. ni hela za serikali, sema serikali imetoa. over.
mwenye ubongo ndivyo ilivyo, asiye na ubongo atakubishia
 
Kwani hiyo miaka 20 unayosema kuhusu Rwanda kuna uongozi wa juu umebadilika halafu mwelekeo wa taifa ukabaki vilevile? Rwanda is has a one man show leadership for over 20 years now.
 

Rais Samia ametoa wapi hizo hela?
Acheni huu ujinga, semeni serikali imetoa hizo hela.
 
Ujinga ni Mzigo. Mh. Rais anatoa wapi hizo Fedha?.??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…