Tanzania kamwe hatutaendelea hivi karibuni ikiwa hatuna mwelekeo wala dira katika uongozi wa nchi. Kila rais ajaye anabuni mambo yake. Baya zaidi ni mambo haya ya kujitakia sifa. Uwanja wa ndege ni huduma/kitega uchumi, haujengwi kwa sababu ya kmuenzi mtu, yeyote. Sidhani kama kuna mtaala wowote uliofanywa juu uwanja huo utarudisha vipi pesa za watoa kodi. Inaelekea pesa za Watanzania zaamuliwa na mhumuko mmoja tu na mapenzi ya mtu! Nchi itaendelea vipi hivyo?
Natoa mfano wa Rwanda: kwa miaka 20 tu iliyopita Rwanda imepiga hatua kubwa sana ya kuigwa. Bila shaka sababu kuu ni kuwa kuna mwelekeo, dira na uongozi usobadilika badilika kama kinyonga.
Pili: Kwa nini kajiwanja kama haka kajengwe na Wachina? Jamani. Inadhi sana. Si muagize vyombo tu msivyonavyo? Mainjinia chungu nzima wapo. Walieni tu nusu ya mnavyowalipa Wachina watafanya kazi zaidi ya Wachina. Mbona Waafrika hatujiamini hivi?