CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Rais Samia atoa wastani wa madarasa manne na madawati 120 katika kila shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima | Hakika awamu ya Sita Tanzania lazima iwe Tanzania.
" Hakuna kama Samaia "
Baada ya janga la Covid-19 kuvuruga Uchumi wa dunia na sisi tukiwemo, Shirika la fedha duniani ( IMF) pamoja na benki ya dunia ( WB) wameanza kuzisaidia nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania mikopo yenye masharti nafuu ili pesa hizo zitumike kama Economic Stimulus & Relief Fund na hapa muelewe vizuri Tanzania tunapokea mikopo na misaada ila "HATUITEGEMEI " ndio maana hata kwenye bajeti yetu hii ya FY2021|22 katia ya Tshs 36.33trl zilizotengwa pesa zetu ni 91.9% huku misaada na mikopo ikiwa ni 8.1% tu,
IMF tayari imeisaidia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kiasi cha Tshs 1.3trl kwaajili ya kusisimua Uchumi wake uliodorora kwasababu ya covod-19 kwani niukweli usiopingika Tanzania tumeumizwa zaidi kwenye Sekta za Utalii,biashara na Usafirishaji,
Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutumia pesa hizo na baada ya kutoa madarasa ya kisasa elfu 15 sawa na wastani wa madarasa manne kwenye kila shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima huku kipaumbele kikiwa ni shule zenye upungufu wa madarasa lakini furaha iliyoje Rais wetu ametoa tena jumla ya madawati 462,795 ambayo ni sawa na Wastani wa madawati 120 kwenye kila Shule ya Sekondari nchi nzima ambazo jumla ya shule hizo ni 3,863.
Sababu za Rais Samia Suluhu Hassan kutoa madarasa mapya manne ya kisasa na madawati mapya 120 katika kila shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima ni kuhakikisha wazazi wa watoto watakaojiunga na kidato cha kwanza mwakani katika mwaka wa masomo 2021|2025 hawalipi hata Shilingia mia moja kwani Rais wetu mnyenyekevu ameshalipa pia ada za watoto wote 1M wanaotakiwa kuanza shule siku moja nchi nzima yaani trh 06|01|2022,hii haijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu,
VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA