Rais Samia atoa wastani wa madarasa manne na madawati 120 katika kila shule ya Sekondari nchi nzima

Hivi Huyo samia anatoa hela zake mfukoni? au ni hii hii tunayokatwa kodi?
Vyovyote itakavyokuwa,sisi wananchi wa kawaida,tunataka maendeleo.Watoto wakiwa na njaa,mama akileta chakula,hatuulizi katoa wapi,sisi bora tushibe
 
Ishu ni Mkopo. Tumeshindwa kufanya hayoyote kwa makusanyao ya kodi, hadi IMF watukopeshe. Hebu niambie ni sekta ipi ambayo serikali kwa 100% inatumia makusanyo yake ya kodi
Bora tushibe,pesa itoke kokote,madhali ajira zitakuwa nyingi.Hapo kuanzia,mafundi,wauza vifaa vya ujenzi,wauza mbao,misumari,vibarua,wachora ramani,mama lishe,wenye virukuu,wamachinga,wauza sokoni,wote watapata pesa.
 
Umesema kweli tupu.
Ndio maana hatutaendelea kamwe kazi kusifia sijui mwalipwa ngapi!
Hizi ni fedha za hao tunaowaita majina yasiyoeleweka.
Kwani bajeti ya hizi wizara inafanya kazi gani? Ndio hapo zinapigwa kimyakimya.
Hamna shida zinunuliwe kwa wingi kwa manufaa.
Vipi na Fire trucks kwani vinaenda sambamba na huduma ya uokoaji?

Tuamke Katiba Katiba ni kipaumbele!


Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
😍😍😍😍 Nchi tajiri sana na inajiweza

Kuihudumia bajeti kwa zaidi ya 90% sio mchezo

#KAZIIENDELEE KWA KASI &WELEDI ZAIDI
Hii nchi ni ya ovyo sana yanazungumzwa mengine tofauti na uhalisia...mnasema nchi ni tajiri sana Ila mikopo kila siku mnaichukua....halafu mambo ya kusema "rais atoa" tulishayakataa semeni "serikali yatoa"
 
Hii nchi ni ya ovyo sana yanazungumzwa mengine tofauti na uhalisia...mnasema nchi ni tajiri sana Ila mikopo kila siku mnaichukua....halafu mambo ya kusema "rais atoa" tulishayakataa semeni "serikali yatoa"
Kwani kunatofauti gani kati ya Serikali na Rais,
 
Kwenye bajeti kuna sehemu ya mikopo pia Chief,
 
Ametoa kwenye mshahara wake au?![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
nimeona moyo wa uzalendo na uthubutu wa Mama yetu Samia Suluhu Hassan katika kutuletea maendeleo Wa Tanzania.
Hakika Tanzania inakwenda kupiga hatua kubwa katika Sector ya afya elimu na Maji.[emoji120][emoji120]
 
Kazi iendelee
 
Huyu mtu CM1774858 sijui analipwa ngapi? lakini at least ana news positive hata kama anaongeza chumvi kiasi, kuna yule wa youtube anaitwa Musiba wakati wa Magufuli that guy was very negative na kazi yake kutishia watu tuu, nafikiri alikuwa anajiona untouchable
 
nimeona moyo wa uzalendo na uthubutu wa Mama yetu Samia Suluhu Hassan katika kutuletea maendeleo Wa Tanzania.
Hakika Tanzania inakwenda kupiga hatua kubwa katika Sector ya afya elimu na Maji.[emoji120][emoji120]
Nikweli kabisa mkuu,

Tuendelee kumpigania,
 
Mkuu naongeza chumvi gani?

Bahati mbaya sana sifahamiana na kiongozi yoyote wa ngazi ya juu,

Mimi ni mwanachama tu mtiifu mwenye Uzalendo kwa nchi yangu,

Nakusihi nawewe uniunge mkono katika hili,

Nimbaya sana kuisemea nchi yako mabaya na kuiombea mabaya


#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…