Rais Samia atua Afrika Kusini kushiriki uapisho wa Ramaphosa hapo kesho

Rais Samia atua Afrika Kusini kushiriki uapisho wa Ramaphosa hapo kesho

Ok, Nimesikia chokochoko huko Bungeni.
Wabunge wa CCM mnafikia pahala mnavuana nguo hadharani .

Mh.Spika ,hili nalo mliangalie wenyewe.
Naamini utaliweza mana una elimu nzuri ya sharia .

Rubani washa ndege tuondoke zetu.
Spika na yule bibi kuwaweka kwenye vyombo vikuu vya maamuzi, ni hatari na hasara ya nchi hii.
 
Mkuu hata hao ni watanzania, nao wanastahili kula keki ya Taifa, chuki dhidi ya watanganyika wenzetu ya nini.

Ndugu Nyabhingi, nguvu Rais kufanya atakavyo na apendavyo tunampa sisi wenyewe kupitia sheria wanazo tunga wabunge wetu.

Tutulie, usilalamikie!!!

⚖️4Asimwe#
Mimi sikiwapigia kula wale mazuzu waliopo bungeni.
Unapata wapi ujasiri wa kuandika kuwa nguvu ya haya maujinga nimewapa mimi!!
Anyways,tungekuwa hata nusu ya energy ya wakenya tungekomesha huu ujinga sababu viongozi wa nchi hii ni waoga sana.
 
Hapo mi sielewi,na ndege yake ipo,ila ye anakwea hilo pipa la abiria 500.
Huku abiria ndege zinaahirishwa kila kukicha.na hilo dubwasha linakunywa mafuta haswa kila likinyanyuka.
Ndege zote ni mali yetu watanzania na Rais wetu anaweza na yupo huru kutumia usafiri na ndege yoyote ile atakayo.
 
Ila kama kufaidi huyo mwewe amefaidi, naona sasa imekuwa kama mwewe wa rais...
 
Waswahili na shughuli !!!wao wanakwambia shughuli ni watu 🤣🤣🤣🤣
Haya mama sisi utatukuta nyumbani tupo hapa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan ametua kwa kishindo na salama kabisa Nchini Afrika kusini,ambako amekwenda kwa ajili ya kuhudhuria uapisho wa Rais wa Taifa hilo Mheshimiwa Ramaphosa utakaofanyika siku ya kesho.

Hii ni baada ya kupata ushindi wa kura takribani 283 baada ya kuungana na chama cha DA(Demoratic Alliance)zidi ya mgombea wa kutoka chama cha EFF cha Julius Malema.ikumbukwe ya kuwa safari hiyo ni ya muhimu sana kwa Rais wetu kuhudhuria,hasa kwa kuzingatia historia yetu ya kipekee kabisa na Taifa letu na Afrika kusini.

Ndio maana mnakumbuka mwaka 2013 namna Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete namna alivyoshangiliwa kwa kishindo na wa Afrika kusini wakati wa msiba wa hayati Nelson Mandela wakati akitoa historia yetu na yeye na namna Tanzania ilivyo msaidia Nelson Mandela katika masuala mbalimbali,hadi akawatania kuwa alisahau viatu vyake na alikuwa akitumia paspoti yetu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

PIA SOMA
- Rais Samia kwenda Afrika Kusini kwenye uapisho wa Ramaphosa


Yule jemba mvaa hijab leo hajaenda kutalii 😂😂😂
 
Back
Top Bottom