Rais Samia atua Chuo cha Taifa cha Ulinzi na kutoa Mhadhara juu ya Falsafa yake ya 4R katika kuongoza serikali yake

Rais Samia atua Chuo cha Taifa cha Ulinzi na kutoa Mhadhara juu ya Falsafa yake ya 4R katika kuongoza serikali yake

Four R zipi?

maridhiano (Reconciliation), mabadiliko (Reforms),
ustahimilivu (Resilience) na
kujenga upya (Rebuilding)

Mbona naona 2m and uk
 
Itapendeza kama Dr Samia awe keynote speaker au atoe presentation ama public lecture kwenye vyuo mbalimbali kuhusu strategic development plan. Amoe kafulila au dr aliyekuwa esrf amuamdalie presentation. Iwe na takwimu, projections na expected results.
Angeanza na Uongozi intitute, NDC, CFR, Udms, mzumbe, TIA, Mwl Nyerere uni of technology haya mambo kagame anayafanya sana ndani na nje ya Rwanda anaalikwa
 
Rais Samia anaweza kufanya mhadhara mahali popote pale
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi,Rais anayeheshimika na kupendwa na watanzania kwa kiwango cha juu utafikiri pesa,hii leo ametua na kuingia ndani ya chuo cha Taifa cha Ulinzi na kupata mapokezi mazito kwelikweli na ya heshima ya hali ya juu sana.

Ambapo akiwa chuoni hapo Mheshimiwa Rais wetu mpendwa ameweza kutoa Mhadhara Mzito sana wa uzani wa juu na kidunia juu ya Falsafa yake ya 4R katika kuongoza serikali yake.ikumbukwe falsafa hiyo ndio imeshuhudia na kuwawezesha wapinzani na vyama vyote vya siasa kupanda majukwaani na kufanya siasa.

Ni kupitia falsafa hiyo imewezesha wapinzani waliokuwa wamekimbia nchi na kuishi uhamishoni kuweza kurejea Nchini kifua mbele na kuishi nchini mwao bila hofu wala wasiwasi,ni kupitia falsafa hizo tumeshuhudia umoja wa kitaifa ukiimarika na kuwa na nguvu kuliko wakati wowote ule.

Ni kupitia falsafa hiyo leo hii hakuna Mwanasiasa ambaye yupo gerezani kwa kesi ya kisiasa, wala kufungwa pingu kwa maonezi na kusafirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, wala mtu kulala na wasiwasi ya kugongewa na kuvunjiwa mlango na hatimaye kukamatwa usiku wa manane kama Jambazi sugu la mauaji.

Ni kupitia falsafa hiyo tumeshuhudia vyama vya siasa hapa nchini vikikaa kwa pamoja katika meza moja ya mazungumzo kunywa maji na kula chakula kwa pamoja na kuzungumza masuala mbalimbali juu ya mstakabali wa Taifa letu na mwisho kupeana mikono kwa amani na upendo.

Ni kupitia falsafa hiyo tumeshuhudia umoja, mshikamano,upendo na udugu ukiongezeaka na kuimarika sana miongoni mwa Watanzania pamoja na kuongezeka kwa moyo wa uzalendo kwa Taifa letu na kupendana sisi kwa sisi bila kujali itikadi zetu za kisiasa.ndio sababu kazi zinaendelea vyema, maendeleo yanapatikana kila Secta,uchumi wetu unakua kwa kasi,watalii wanaendelea kumiminika nchini kufikia millioni 1.8,mapato yanaendelea kuongezeka,biashara zinaendelea kuongezeka.

Ni kupitia falsafa hiyo tunaona Amani na utulivu vinaendelea kutamalaki na kushamiri hapa nchini.hiyo yote ni kazi ya Mikono ya Jemedari wetu na Rais wetu mpendwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan jasiri muongoza njia na shujaa wa Afrika,mama wa shoka,chuma cha Reli kiongozi imara na hodari katika uongozi.hii yote ni akili ,upeo na maarifa makubwa ya kiuongozi aliyo nayo Rais wetu kipenzi.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Sijamaliza hata kusoma hili andiko lako la chooni, ila fikra za vijana Kama wewe imenifanya niamini hili taifa watu wanaugua ugonjwa wa akili bila kujijua.
 
Mnajuana nyie!
Kwanini huwezi kuishi humu jf bila yeye? Kwanini unampenda wewe na Benjamini
Jana ulimmiss wewe😂🤸
Ni mwana ila anazingua sana, jana nilimrushia kiteni ndiyo akaingia humu,dogo ni mkuda sana.
 
Ni mwana ila anazingua sana, jana nilimrushia kiteni ndiyo akaingia humu,dogo ni mkuda sana.
Ukimjua mtu hakupi shida
Lucas anachangamsha jukwaa la siasa tumuache, akiondoka tutammiss huyu😂
 
Nyie chadema mna akili fupi yaani mtu akimkubali rais samia bhc ni chawa ,,sasa mm mtanzania na samia ndio rais wetu kwann nimkatae ,samia 2025 atapita na mtabaki na chuki zenu mpk mpate ugonjwa wa moyo maana kukaa na kinyongo kwa miaka 10 c mchezo
 
Nyie CCM hamna akili kabisaaaaa
 
Back
Top Bottom