Izato
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 5,441
- 11,669
Anakwenda kujichoresha tu mbele ya viongozi wenzake. Kila mtu anamjua ni mwizi wa kura, aliyejiweka madarakani kwa njia haramu, muuaji wa raia wake, na Tundu Lissu yupo korokoroni kwa kesi ya uongo!Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Ametua kwa kishindo kikuu kilicho itetemesha Ardhi ya Adis Ababa Ethiopia katika kushiriki na kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali.
Lakini pia Rais wetu anapendekezwa Kutangazwa kama kinara wa kupigania Afya ya Mama na Mtoto. Ikumbukwe Mama yetu Mpendwa amefanya kazi kubwa sana katika kuimarisha huduma ya Mama na mtoto.
Jambo ambalo limepunguza vifo vya Mama na mtoto. Hii imefanyika kwa kuongeza Bajeti ya Afya ,kuboresha huduma za afya ,kujenga vituo vya afya kwa wingi, kutoa Elimu na kununua vifaa tiba na Madawa ya kutosha katika mahospitali mbalimbali nchini.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.View attachment 3543007View attachment 3543009
She is real a Laughing stock