Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Rais Samia akipokea Tuzo Maalum kutoka Bungeni Dodoma Mei 31, 2025
View: https://www.youtube.com/live/dtSWOacZX3s?si=52R5DMNF-khUWAEl
=============================================================
Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania akizungumza wakati Bunge likikabidhi tuzo maalum kwa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema
"Leo tunajivunia Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambao umeakisi utawala bora, weledi, uwajibikaji, uaminifu na ujumuishi, umekuwa kiongozi wa mfano, katika kuimarisha mifumo ya sheria, haki za binadamu, na uwazi unaozingatia usawa, na maendeleo ya kila mwananchi"
"Kwa nafasi yetu wabunge tumeshughudia historia ya mafanikio na mabadiliko yaliyoleta tija na ustawi kwa jamii nzima, leo Mheshimiwa Rais tunapokusanyika hapa tunaadhimisha na kutambua mchango wako, kupitia tuzo hii maalum"
"Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo linakutunukia tuzo kwa kutambua mchango mkubwa ambao umeutoa kuhakikisha Tanzania inashiriki kwa ujumla wake katika kuleta maendeleo duniani"
"Wabunge hawa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kutafakari nini cha kufanya kwa niaba ya wananchi wanaowawakilisha, wakawaza kukupa tuzo maalum leo"
"Kama isingekuwa muda katika majimbo yote ya Tanzania ambayo yapo 264 na sasa yameongezeka ambayo wabunge wake hawajaja bado bungeni, wabunge hawa kila mmoja wao anayo hadhithi njema ya kutoka kwenye majimbo yao na kazi uliyofanya katika sekta zote"
Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo maalum na Bunge la Tanzania amesema
"Nimefarijika kuungana nanyi leo kwani ni mara yangu ya pili kujumuika nanyi tangu nikabidhiwe dhamana ya uendeshaji wa nchi yetu, nami nikiwa zao la bunge hili bado nina kumbukumbu nzuri ya uwepo wangu ndani ya bunge, nalikumbuka sana bunge la kumi (2010 mpaka 2015) na lile la Katiba la 2014, yalivyonilea, kuniongoza na kunipika vyema mpaka kufikia hatua hii niliyo sasa"
"Kwa niaba ya wenzangu katika Utumishi wa umma, tunamshukuru Mungu kwakuwa kazi inayofanyika inatambuliwa na kuthaminiwa na Bunge hili adhimu. Wabunge mkiwa ni wawakilishi wa wananchi ni kusema kwamba wananchi wa Tanzania wamethamini kazi inayofanywa na Serikali yao."
"Nyote ni mazingira yalivyokuwa wakati naipokea nchi, mazingira ya kiuchumi hayakuwa vyema kwa ulimwengu mzima ulimwengu mzima kutokana na maradhi yale ya Covid 19, mazingira ya kijamii yalikuwa na fadhaha kubwa, kwanza ya maradhi, lakini fadhaha ya kuondokewa na mpendwa wetu Rais aliyekuwa Madarakani, na mazingira ya kisiasa hayakuwa na bashasha kwa kuwa haikuwa muda mrefu tangu tumemaliza uchaguzi wa 2020"
"Kwa hiyo kwa mazingira yote hayo kwa hali yoyote ile, kwa mtazamo wa mwanadamu, mja wa kuupokea mzigo ule wa Urais kwa wakati ule kwa mazingira yale isingefikiriwa kwamba ningekuwa mimi, ila kwa ukuu wa katiba yetu ya Tanzania hakukuwa na budi ila kukabidhi madaraka yake kwa aliyekuwa Makamu wa Rais"