PreGE2025 Rais Samia atunukiwa Tuzo Maalum kutoka kwa bunge, Dodoma Mei 31, 2025

PreGE2025 Rais Samia atunukiwa Tuzo Maalum kutoka kwa bunge, Dodoma Mei 31, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
" Leo nimepata heshima kubwa ya kutunukiwa Tuzo Maalum ya Heshima na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama njia ya kutambua kazi kubwa inayoendelea kufanywa kuimarisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa. Sauti ya Bunge ni sauti ya wananchi. Ahsanteni sana.

Hakika, kidole kimoja hakivunji chawa. Mafanikio tunayojivunia leo si nguvu, uhodari au maarifa yangu pekee, bali ni matokeo ya mipango mbalimbali ya nchi yetu na maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025. Aidha, ni matunda ya kazi kubwa inayofanywa na Bunge letu ya kuisimamia na kuishauri Serikali.

Nimepokea tuzo hii kwa niaba ya Watanzania wote. Ninawashukuru nyote kwa kazi kubwa tunayoendelea kuifanya kwa pamoja kuleta maendeleo kwa Taifa letu, huku tukibaki kuwa wamoja, wenye amani na mshikamano."
 

Attachments

  • IMG-20250531-WA0008.jpg
    IMG-20250531-WA0008.jpg
    119.5 KB · Views: 20
" Leo nimepata heshima kubwa ya kutunukiwa Tuzo Maalum ya Heshima na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama njia ya kutambua kazi kubwa inayoendelea kufanywa kuimarisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa. Sauti ya Bunge ni sauti ya wananchi. Ahsanteni sana.

Hakika, kidole kimoja hakivunji chawa. Mafanikio tunayojivunia leo si nguvu, uhodari au maarifa yangu pekee, bali ni matokeo ya mipango mbalimbali ya nchi yetu na maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025. Aidha, ni matunda ya kazi kubwa inayofanywa na Bunge letu ya kuisimamia na kuishauri Serikali.

Nimepokea tuzo hii kwa niaba ya Watanzania wote. Ninawashukuru nyote kwa kazi kubwa tunayoendelea kuifanya kwa pamoja kuleta maendeleo kwa Taifa letu, huku tukibaki kuwa wamoja, wenye amani na mshikamano.
Anastahili
 
Rais Samia akipokea Tuzo Maalum kutoka Bungeni Dodoma Mei 31, 2025


View: https://www.youtube.com/live/dtSWOacZX3s?si=52R5DMNF-khUWAEl
=============================================================

Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania akizungumza wakati Bunge likikabidhi tuzo maalum kwa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema

"Leo tunajivunia Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambao umeakisi utawala bora, weledi, uwajibikaji, uaminifu na ujumuishi, umekuwa kiongozi wa mfano, katika kuimarisha mifumo ya sheria, haki za binadamu, na uwazi unaozingatia usawa, na maendeleo ya kila mwananchi"

"Kwa nafasi yetu wabunge tumeshughudia historia ya mafanikio na mabadiliko yaliyoleta tija na ustawi kwa jamii nzima, leo Mheshimiwa Rais tunapokusanyika hapa tunaadhimisha na kutambua mchango wako, kupitia tuzo hii maalum"

"Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo linakutunukia tuzo kwa kutambua mchango mkubwa ambao umeutoa kuhakikisha Tanzania inashiriki kwa ujumla wake katika kuleta maendeleo duniani"

"Wabunge hawa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kutafakari nini cha kufanya kwa niaba ya wananchi wanaowawakilisha, wakawaza kukupa tuzo maalum leo"

"Kama isingekuwa muda katika majimbo yote ya Tanzania ambayo yapo 264 na sasa yameongezeka ambayo wabunge wake hawajaja bado bungeni, wabunge hawa kila mmoja wao anayo hadhithi njema ya kutoka kwenye majimbo yao na kazi uliyofanya katika sekta zote"



Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo maalum na Bunge la Tanzania amesema

"Nimefarijika kuungana nanyi leo kwani ni mara yangu ya pili kujumuika nanyi tangu nikabidhiwe dhamana ya uendeshaji wa nchi yetu, nami nikiwa zao la bunge hili bado nina kumbukumbu nzuri ya uwepo wangu ndani ya bunge, nalikumbuka sana bunge la kumi (2010 mpaka 2015) na lile la Katiba la 2014, yalivyonilea, kuniongoza na kunipika vyema mpaka kufikia hatua hii niliyo sasa"

"Kwa niaba ya wenzangu katika Utumishi wa umma, tunamshukuru Mungu kwakuwa kazi inayofanyika inatambuliwa na kuthaminiwa na Bunge hili adhimu. Wabunge mkiwa ni wawakilishi wa wananchi ni kusema kwamba wananchi wa Tanzania wamethamini kazi inayofanywa na Serikali yao."

"Nyote ni mazingira yalivyokuwa wakati naipokea nchi, mazingira ya kiuchumi hayakuwa vyema kwa ulimwengu mzima ulimwengu mzima kutokana na maradhi yale ya Covid 19, mazingira ya kijamii yalikuwa na fadhaha kubwa, kwanza ya maradhi, lakini fadhaha ya kuondokewa na mpendwa wetu Rais aliyekuwa Madarakani, na mazingira ya kisiasa hayakuwa na bashasha kwa kuwa haikuwa muda mrefu tangu tumemaliza uchaguzi wa 2020"

"Kwa hiyo kwa mazingira yote hayo kwa hali yoyote ile, kwa mtazamo wa mwanadamu, mja wa kuupokea mzigo ule wa Urais kwa wakati ule kwa mazingira yale isingefikiriwa kwamba ningekuwa mimi, ila kwa ukuu wa katiba yetu ya Tanzania hakukuwa na budi ila kukabidhi madaraka yake kwa aliyekuwa Makamu wa Rais"
​
 

Attachments

  • IMG-20250531-WA0008.jpg
    IMG-20250531-WA0008.jpg
    119.5 KB · Views: 18
Mwenyekiti wa CCM kutunukiwa tunzo ktka kikao cha chama chake sio jambo la kushangaxa
 
Angejua yeye na Hilo bunge la mchongo wanavyochukiwa huku mtaani Wala wasinge mkejelisha hivyo. Katikati ya vilio na majonzi ya watanzania juu ya utekaji halafu unapewa tuzo hujui kwamba hiyo ni bad timing na wenye akili wanakuchora Samia.
 
Kila siku kabla ya kulala nyosha mikono juu sema "nchi ya kipumbavu sana hii."
 
Wazungu wanapotuitaga watu weusi nyani huwa tunakasirika sana ila kuna muda inabidi tukubali tu kuwa Watu weusi hasa Watanzania hatuna tofauti na manyani kiakili na kiupeo.

Kikawaida tu, Chama kinaomba ridhaa ya kuongoza watu , kinakuwa na ilani, kinatekeleza ilani kama wajibu wake alafu baada ya kutekeleza ilani, anapewa tuzo Rais, tena na Bunge ambalo lina wajibu wa kumsimamia ili atekeleze hiyo Ilani na anayoahidi.

Cha kushangaza zaidi hayo yote yanayodaiwa kutekelezwa sio kwamba yametekelezwa kwa fedha binafsi za huyo Rais bali kwa kodi za Wananchi Masikini ambao kimsingi wanalipa hizo kodi ili wapate hizo huduma maana kodi ni lazima ilipwe ili mtu apate huduma.

Kuna upuuzi duniani unaukuta Tanzania tu. Sijui tulimkoseaga Mungu nini?
Mkuu kilichofanyika nalinganisha na mtu kujitekenya mwenyewe alafu anacheka. Kweli Africa nyeusi haing'oi nanga.
 
Back
Top Bottom