PreGE2025 Rais Samia atunukiwa Tuzo Maalum kutoka kwa bunge, Dodoma Mei 31, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
" Leo nimepata heshima kubwa ya kutunukiwa Tuzo Maalum ya Heshima na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama njia ya kutambua kazi kubwa inayoendelea kufanywa kuimarisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa. Sauti ya Bunge ni sauti ya wananchi. Ahsanteni sana.

Hakika, kidole kimoja hakivunji chawa. Mafanikio tunayojivunia leo si nguvu, uhodari au maarifa yangu pekee, bali ni matokeo ya mipango mbalimbali ya nchi yetu na maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025. Aidha, ni matunda ya kazi kubwa inayofanywa na Bunge letu ya kuisimamia na kuishauri Serikali.

Nimepokea tuzo hii kwa niaba ya Watanzania wote. Ninawashukuru nyote kwa kazi kubwa tunayoendelea kuifanya kwa pamoja kuleta maendeleo kwa Taifa letu, huku tukibaki kuwa wamoja, wenye amani na mshikamano."
 

Attachments

  • IMG-20250531-WA0008.jpg
    119.5 KB · Views: 20
Anastahili
 
 

Attachments

  • IMG-20250531-WA0008.jpg
    119.5 KB · Views: 18
Mwenyekiti wa CCM kutunukiwa tunzo ktka kikao cha chama chake sio jambo la kushangaxa
 
Angejua yeye na Hilo bunge la mchongo wanavyochukiwa huku mtaani Wala wasinge mkejelisha hivyo. Katikati ya vilio na majonzi ya watanzania juu ya utekaji halafu unapewa tuzo hujui kwamba hiyo ni bad timing na wenye akili wanakuchora Samia.
 
Kila siku kabla ya kulala nyosha mikono juu sema "nchi ya kipumbavu sana hii."
 
Mkuu kilichofanyika nalinganisha na mtu kujitekenya mwenyewe alafu anacheka. Kweli Africa nyeusi haing'oi nanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…