PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Uongozi uliopita uliokuwa unatuhumiwa kwa mambo kama ya sasa na kudhoofisha mifumo ya haki ndio waje kufanya uchunguzi wa mauji haya yaliyofanyika kwenye serikali ya sasa (yako)? Juma, Tax, Mwema ndio the best you could do kweli?

Ripoti iliyotolewa na Jaji Chande juu ya ukatili wa polisi imefanyiwa nini mpaka leo? Rais Samia unawatanzania Watanzania ambao uvumilivu wao kwenye maumivu umebakia utambi tu halafu unaenda kutia kijiti machoni!

Lakini tume hii imewekwa na majina tu, haina vitu muhimu;
- Je, kazi hiyo inaanza lini?
- Ni yapi majukumu ya kila mmoja katika tume hii?
- Kazi ya tume hii inaisha lini?


La muhimu kabisa KWANINI IMEFICHWA KUWA TAX ALIWAHI KUWA WAZIRI WA ULINZI, ambaye chini yake aliwahi kutoa maagizo ya kipumbavu ili wanchi wafanyiwe ukatili na kuuliwa? Ili aonekane Mwanadiplomasia mbobevu wakati ni juzi tu hapo alisema akina Agather na mwenzake aashughulikiwe? Muuaji akamchunguze muuaji?!

Lakini hapo nyuma iliundwa tume ya haki jinai na ikaja na mapendekezo mazuri tu ambayo yangefanyiwa kazi tusingefika hapa na kushuhudia mauaji mabaya kabisa kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu.

Hii ripoti kuna ulichotekeleza Samia - Tume ya Haki Jinai: TAKUKURU ina watumishi Wala Rushwa na Wasio Wabobevu

Haya ni matokeo ya kuuza matokeo ya tume zote hizo, na wakulaumiwa ni wewe SAMIA.



=====

TAARIFA KWA UMMA​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, ameunda Tume Huru ya kufanya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.

Aidha, Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo na wajumbe walioteuliwa ni wafuatao:-

(i) Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania;

(ii) Balozi Ombeni Yohana Sefue Kiongozi Mstaafu; Mwanadiplomasia na Katibu Mkuu

(iii) Balozi Radhia Msuya - Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu;

(iv) Balozi Lt. Gen. Paul Meela - Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu;

(v) IGP (Mstaafu) Said Ally Mwema Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Mstaafu;

(vi) Balozi David Kapya - Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu; na(vii) Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax Aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi,

Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka
KATIBU MKUU KIONGOZI
18 Novemba, 2025​

Screenshot_20251118_165140_Instagram.jpg

IMG_0205.jpeg


Fuatilia kilichojiri baada ya kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya Oktoba 29, 2025
 
Back
Top Bottom