PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kiwemo Mama yako ndio utaona ya maana.
Sasa wanajichunguzaje wenyewe? Anaacha kuchukua wachunguzi kutoka nje anachukua genge lake wamchunguze wewe unafikiria ungekua wewe ungemletea majibu gani kwa mfano, yaan tuseme ameua na wewe huyo ndio boss wako halafu anakwambia nichunguze halafu niletee majibu wewe ukishachunguza utampelekea majibu gani labda kwa mfano kwamba boss uchunguzi unaonyesha wewe ndio umeua?
 
Uongozi uliopita uliokuwa unatuhumiwa kwa mambo kama ya sasa na kudhoofisha mifumo ya haki ndio waje kufanya uchunguzi wa mauji haya yaliyofanyika kwenye serikali ya sasa (yako)? Juma, Tax, Mwema ndio the best you could do kweli?

Ripoti iliyotolewa na Jaji Chande juu ya ukatili wa polisi imefanyiwa nini mpaka leo? Rais Samia unawatanzania Watanzania ambao uvumilivu wao kwenye maumivu umebakia utambi tu halafu unaenda kutia kijiti machoni!

View attachment 3503744
JamiiCheck
 
Upumbavu mtupu, Utekaji, mauaji, Ufisadi, rushwa, uminywaji wa democrasia ni vitu vya kuundiwa tume kweli? Kwa hiyo mnaona watanzania ni wajinga mnaendelea kuwachchoea D9 hiyo Tume inaundwa na mtuhumiwa inapeleka majibu kwa huyo huyo mtuhumiwa mkuu 😂😂😂
 
Back
Top Bottom