Rais Samia aunda Tume za Rais za Kutathmini Mgogoro wa Ardhi Hifadhi ya Ngorongoro na Kutathmini Zoezi la Uhamaaji wa Hiari katika Hifadhi

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
photo_2024-12-23_21-51-04.jpg

Tarehe 01 Desemba, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokutana na viongozi wa kimila na jamii ya kimasai wanaoishi eneo la Hifadhi ya Ngorongoro alitangaza uamuzi wa Serikali kuunda Tume mbili ambapo Tume ya Kwanza itafanya tathmini kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na Tume ya Pili itaangalia utekelezaji wa zoezi la uhamaiji wa hiari kutoka eneo la Hifadhi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Dkt. Samia ameunda Tume ya Rais ya Kutathmini kuhusu Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro na kumteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Dkt. Gerald Ndika kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo. Aidha, wajumbe wa Tume walioteuliwa ni wafuatao:

(i) Bw. Philemon Luhanjo - Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu;
(ii) Bi. Zakia Hamdani Meghji - Aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii;
(iii) Jaji George Mcheche Masaju - Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais, Sheria;
(iv) Dkt. Richard Muyungi - Mshauri wa Rais, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi;
(v) Balozi Salome Sijaona - Balozi na Katibu Mkuu Mstaafu;
(vi) Prof. Wilbard Kombe - Profesa wa Chuo Kikuu Ardhi;
(vii) Prof. Emmanuel Luoga - Profesa wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo;
(viii) Bw. Mollel James Moringe - Diwani na Katibu wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro;
(ix) Bi. Moi Aprakwa Sikorei - Diwani na Mkazi wa Ngorongoro.

photo_2024-12-23_21-50-57.jpg
 
Ngorongoro imemulikwa sana nahisi Kuna kitu nyumba ya pazia. Ukiona mzinga wa nyuki ni wakali ujue Kuna asali.
 
Back
Top Bottom