Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Wacha siku mbili hizi presha na sukari ziwaaamke kidogo 😂😂

Wakae vikao vya gizani kusolvu mambo ila wapi....

Watu mtaani kupata hata milo mitatu ya ovyo ni shida...

Wachomwe moto 😳
 
Rais aliruhusu watu wale kwa urefu wa kamba zao kwa nini hawa amewatengua.?Na kama kweli anauchungu na nchi kwa nini makamba hajamtumbua licha wizara yake inanuka ufisadi?
 
Sasa kwanini Rais akaagiza hao makatibu wakuu wawachunguze wa chini yao na ikibidi hatua dhidi yao zichukuliwe?

Inawezekana vipi hao wasaidizi kufanya jambo bila kushirikishwa makatibu wakuu? na kama makatibu wakuu walishirikishwa, kwanini wawachunguze hao wasaidizi ikiwa nao ni sehemu ya tatizo?
Katibu mkuu ndiye msimamizi mkuu, wa taasisi zote zilizo chini ya wizara yake na ana wajibu wa kupitia hoja za CAG na kuzipatia majibu....

Muelewe ripoti ya CAG huachs hoja ambazo huhitaji majibu ikiwa tofauti ndipo hatua huchukuliwa.
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?

Yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe wakiwemo mawaziri?

Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, sioni jipya, kapanua magoli hao jamaa wapate visingizio.
Ulitaka Rais afanye nn kwani?
 
Kulingana na taarifa ya Ikulu ikiwaelekeza watu hao kusoma report ya CAG na kuchukua hatua kwa wahalifu imekaaje?
Naona kama mbwa kala mbwa !
Maruweruwe hapa sielewi!
Badala ya kuagiza TAKUKURU wanagizwa wakurungenzi!
IMG-20230409-WA0039.jpg
 
Bado haitakuwa suluhisho.
Moja ya suluhisho kubwa ni kumpunguzia rais madaraka makubwa aliyonayo ikiwemo madaraka ya kuteua ma CEOs karibu wote. Madaraka haya yapunguzwe yapelekwe bungeni na kwenye mhimili wa mahakama....maana yake hapo ni katiba mpya.
Tumlaumu Nyerere
 
Vipi kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe na ubadhirifu, mamlaka yao ya uteuzi na nidhamu ni nani?

Hivi unategemea hao wakuu watakuwa tayari kuwatoa sadaka wasaidizi wao watakaobainika kufanya uzembe?

Sababu kwa akili ya kawaida tu, kama wasaidizi wakibainika kusababisha uzembe, swali litakuja, je, wakuu wao walikuwa wapi hadi huo uzembe kutokea?

Alichofanya Rais hapa ni muendelezo wa kulindana, sioni jipya; wakuu watawalinda wasaidizi wao waliofanya uzembe, kama ambavyo Rais nae anawalinda wakuu wao waliosimamia uzembe, mwishowe mbwa mwitu wataendelea kututafuna kila siku.
Usiwe na haraka basi!Da!Katibu Mkuu na Makatibu yeye na Mawaziri tusubiri tuone.Haraka ya Nini Kamanda.
 
huyu mkurugenzi wa wakala wa ndege za umma ndio alihusika kipandisha bei ndege ya mizigo invoice ikaja mlima wa pesa
Hawezi jiamlia tu kuna wakubwa wameamua wamtoe kafara
 
TAKUKURU sio independent wanashakizwa kukamata vidagaa.

Ila rais anakusanya maoni ipo siku hii itakuwa independent maana wamemchezea na kashawaelewa.
 
Huyu bwana anahusika na ununuzu wa ndege za ATCL? Bodi na management za ATCL hazihusiki?
Huyo ndio mhusika mkuu, TGFA ndiye mnunuzi kwa niaba ya serikali, ndege zinaponunuliwa anasaini yeye upande mmoja na mtendaji wa ATCL upande mwingine.
 
Hii maana yake Rais haoni tatizo, anaelekeza kitu gani ambacho yeye hakioni?

Naona mnatumia kigezo cha "utaratibu na sheria" ili kuzubaisha watu, na kulindana tu, na bahati nzuri kwasababu nae hapendi kuhangaisha kichwa chake ...

Marehemu Abeid Amani Karume alikuwa na msemo " Ukimkamata mwizi keba , keba tu hakuna jingine ni kumuadabisha tu" Nadhani wakati marehemu anasema hayo Samia alikuwa bado sana!!
 
Mmmm kama kukwepa majukumu hivi! Kuna mtu hataki lawama hapa!
Wakurungenzi na makatibu wakuu ndi wezi sana wa hizi pesa tena wachunguzane wao kwa wao?
TAKUKURU sio independent wanashakizwa kukamata vidagaa.

Ila rais anakusanya maoni ipo siku hii itakuwa independent maana wamemchezea na kashawaelewa.
 
Binafsi naona siyo sawa. Wanaweza wakalindana. Namuomba mhe. Rais Samia pamoja na kuwapa hiyo kazi lkn na yeye afuatilie kwa makini sana
 
Ungekuwa wewe ungefanyaje? Unazijua kazi na majukumu ya katibu mkuu kwenye wizard?
Duh watz wajuaji sana. Sasa hizi si ndio hatua zenyewe jamani ??? Mlitaka Whitwell wanyongwe bila hata kusikilizwa
Sio wote wanaojua kuhusu "principles of natural justice"
 
PCCB wanakuwa huru baada ya hao wahusika kupitia na kuwachomoa
 
Kwani hizi anazochukua sio hatua? Kumbuka Rais Huwa hana mihemko na hataki kumuonea mtu.

Ukweli ukibainika wote wataondoka.
Mkuu hizi ni dana dana tu. Chama ni kile kile Serikali ni ile ile Majizi ni wale wale Bunge ni lile lile kibogoyo. Hakuna jipya.
 
Back
Top Bottom