Rais Samia awaambia walimu kuwa kuna mambo mazuri yanakuja

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Serikali imeahidi neema kwa walimu huku ikiwataka waendelee kufanya kazi kwa moyo.

Ahadi hiyo imetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, leo Februari 7, 2022 wakati aliposimama wilayani Butiama kwa ajili ya kusalimia wakazi wa wilaya hiyo.

"Walimu hoyeee, walimu mpo eehh sasa naomba niwaambie walimu mambo mazuri yanakuja endeleeni kuchapa kazi tumewajengea madarasa mazuri sasa kazi kwenu" amesema bila kufafanua zaidi.

Rais Samia amewataka wakazi wa wilaya ya Butiama kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kujiletea maendeleo huku akisema kuwa Serikali itaendela kushirikiana nao katika kuleta maendeleo.
 
Safi sana
 
Mama anazidi kuupiga mwingi kwenye kupanga maneno matamu ya kiswahili.
 
Mama aongezewe ulinzi, tunataka chopa 6 angazi zilizosheheni makomando toka jwtz wenye silaha na utayari wa mapambano muda wote.
Timu ya madaktari wasiopungua 50 wanaoweza kumtibu akipata tatzo la afya na
Timu kabambe ya mashehe, mapadre na wachungaj ili wamuongoze ktk toba akihtajika na sir god il aende pema pepon.

Mama huyu anauheshm utumish wa uma.

Mei day ijayo atarejesha matumain

Nb.
Mwaka huu amepandisha vyeo kwa watumish weng sana, tena sana.
 
Mimi Kama mwalimu mzoefu Sina hofu kabisa na huyu rais wetu,

Kazi iendelee
 
Hajafukuza mtu kazi leo?
 
Watanganyika wanatiwa moyo..

#MaendeleoHayanaChama
 
Asisahau pia kuna kundi kubwa la wahitimu wa huo ualimu kutoka familia maskini, wanataabika tu mtaani kwa kukosa ajira.

Hivyo haina maana sana kuongeza tu idadi ya madarasa na wanafunzi, huku maelfu ya wahitimu wa hiyo fani ya ualimu wakiachwa mtaani bila ya kazi.
 
Akijitahidi sana ataongeza 24,000/=
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…