Rais Samia awahakikishia Umoja wa Ulaya kuwa na utawala wa kidemokrasia

Rais Samia awahakikishia Umoja wa Ulaya kuwa na utawala wa kidemokrasia

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezungumza na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya(EU), Charles Michel ambapo amemsifu Rais Samia kwa hatua anazochukua kukabiliana na #COVID19.

EU wamesema wako tayari kushirikiana na viwanda mbalimbali vinavyozalisha chanjo ya #COVID19 barani Afrika ikiwemo Tanzania ikiwa itahitaji msaada huo.

Rais Samia amemuhakikishia Rais wa EU kuwa atahakikisha uwepo wa demokrasia katika utawala wake, utawala bora na haki za msingi za binadamu.

1626095993631.png

1626096005152.png
 
Afadhali huyu amehaidi kuendelea kudumisha demokrasia na haki za binadamu na tayari wingu jeupe lilianza kuonekana ndani ya siku zake 100 za Utawala wake kwa kuondoa baadhi ya kesi za kisiasa za kubambika.

Nashauri, apewe muda, mazuri mengi zaidi kutoka kwake yanakuja.
 
Kwa urais wa kurithi sio rahisi atekeleze utawala wa sheria, maagizo yote anapewa na genge aliloacha Magu.
Kuna "...genge aliloacha Magu" lililosalia kwenye muundo alioutengeneza yeye mwenyewe na kuukamilisha hivi karibuni? Hilo genge litakuwa limejificha wapi, ndani ya chama, ambacho yeye mwenyewe ndiye mwenyekiti wake?

Maana ya yeye mwenyewe kung'ang'ania serikali yake itambuliwe kuwa ni "Awamu ya Sita" ni alama tosha ya kutaka asihusishwe na jambo lolote linalotokana na awamu ya tano.

Hakuna genge tena, akivurunda, tumseme yeye kama yeye, na siyo kwa sababu ya genge.
 
Kwa urais wa kurithi sio rahisi atekeleze utawala wa sheria, maagizo yote anapewa na genge aliloacha Magu.
Katiba ndio inasema hivyo?

Je, Samia hana mamlaka ya kuwafukuza hilo genge la Magu?
 
Sisikiii tena yale mambo ya Ushoga mkiyaongea.....naona mnapongezana tu
 
Chadema chama bora Barani Africa

Wale waliokuwa wanabweka bweka Mabeberu wapite Huku
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom