Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Uzur na ubaya sisi ndo tunaona ko tunajua hari ya utumishi ilikuwaje wakati wake na ikoje wakati huu


Wananchi tunaona kwa macho yetu

Yeye anendelee kuamini yesu aliogopwa kwa nidham ya woga
 
Kwamba hii mijadala yenu humu mitandaoni inaipa pressure serikali hii ya ccm? Nimemwambia anitajie jambo moja tu ambalo wabongo mliipa pressure serikali kutokea humu mitandaoni ila hakutaja hata moja.
Akisha kutajia hiyo mijadala utaisadia nini serikali kutatua kero za wananchi ?
 
Hilo neno mihemko unalitumia kama bendera fuata upepo, na unadhani ukilitumia litasaidia kuondoa ukweli uliopo? Hicho nilichosema ndio ukweli, hutaki jinyonge.
Unapoteza sana nguvu zako kwa kubishana na wafuasi wa jiwe maana hata kama utatumia mwaka mzima kuwaelewesha kamwe hawatakubali ukweli utawale.
 
Aliuwa watu wengi?
 
Uzur na ubaya sisi ndo tunaona ko tunajua hari ya utumishi ilikuwaje wakati wake na ikoje wakati huu


Wananchi tunaona kwa macho yetu

Yeye anendelee kuamini yesu aliogopwa kwa nidham ya woga
Siyo yeye tu bali hata kabla ya yeye kuyasema haya hadharani.

Kupitia jukwaa hili hili sisi wapinzani tulisha yasema kitambo kuwa Jiwe anatumia mkono wa chuma kutawala.

Lkn chawa wake wakaja na propaganda kuwa tunao mpinga jiwe ni mafisadi.
 
Utakuwa mjinga mkuu kuamini kosa la mtangulizi litafanya lako kuwa halali.

Kwani huyu anafanya kwa kumuiga mtangulizi wake? Yeye huyu ndio tabia yake ya kuongea, kama kuna mahali itafanana na ya mtangulizi wake ni coincidence, na sio kumuiga yoyote.
 
Yeye mwenyewe alikuwa havai barakoa, baada ya Magu kuondoka anavaa Barakoa!!
Sasa yeye aseme atafanyaje kuendeleza hiyo heshima bila woga?
Haoni kuwa dawa kwa sehemu kubwa ni kupunguza madaraka ya Rais? Yeye alipo hapo anapewa heshima ya woga!!
Ndiyo maana tunapiga sana kelele za kuhitaji katiba mpya ndiyo muarobaini wa hii sarakazi.

Katiba iliyopo sasa hivi pamoja na madhaifu mengine lkn pia inampatia rais madaraka makubwa sana
 
Na maza alikuwa wapi wakati huo?
Alikuwa kwenye kundi hilo lililokuwa linafanya nidhamu ya uoga.

Asingeweza kupinga mawazo ya boss wake na ndiyo maana leo hii ameamua kuyasema hadharani.
 
Akisha kutajia hiyo mijadala utaisadia nini serikali kutatua kero za wananchi ?
Kero zitatatuliwa vp na wakati nyie mnatetea huu utawala, wenzenu wanalalamika kuwa sasa hakuna tena nidhamu kazini ila nyie mnaona sasa ndio sahihi na kusema zamani mlikuwa mnamuogopa Jiwe. Watu kila wakilalamika kero zilizopo nyie mnasema bora hizo kero kuliko kutawaliwa na Magufuli, sasa kero zipi unazozungumzia?
 
Sio kwamba nipo Tanzania tu, pia sipo kwa kubahatisha, hapa nipo kabla hata hujajiunga jf.
Kujiunga jf nako sifa? Toka ulivyojiunga huko zamani hadi leo umeleta tija gani kwenye nchi? Si unapiga kelele tu humu.
 
Jamaa anasema hii mijadala ya humu mitandaoni inaitia pressure serikali hii ya Tz, ndio maana namuuliza yupo hapa Tz kweli?
Ina maana hujawahi kumsikia mama Samia anasema anapitia sana kwenye mitandao na kuona jinsi watanzania wanalalamika?

Umesahau kabisa kuwa Magufuli aliwahi kulalamika juu ya mitandao na akaomba angalau malaika waizime mitandao?

Unadhani kwanini hao viongozi wetu waliamua kuizungumzia mitandao?

Kwa taarifa yako mitandao inatoa pressure kubwa sana kwa watawala .
 
Kujiunga jf nako sifa? Toka ulivyojiunga huko zamani hadi leo umeleta tija gani kwenye nchi? Si unapiga kelele tu humu.
Hizo hizo kelele zake ndiyo zinawanyima watawala usingizi kwani kupitia mitandao wanazipata kero za wananchi
 
Kujiunga jf nako sifa? Toka ulivyojiunga huko zamani hadi leo umeleta tija gani kwenye nchi? Si unapiga kelele tu humu.

Ni sifa kwelikweli, ndio maana ww kila siku uko humu. Kama vipi ondoka ukatolee maoni yako TBC1 maana ww ndio unaijua vizuri Tanzania.
 
Jamaa anasema hii mijadala ya humu mitandaoni inaitia pressure serikali hii ya Tz, ndio maana namuuliza yupo hapa Tz kweli?

Kama mitandao haiitii pressure serikali, kwanini wakati wa uchafuzi wa 2020 serikali ilizima mitandao? Sasa hivi kila serikali ikiongea utasikia kutokana na maoni ya mitandaoni, hii maana yake ni kuwa kwenye mitandao ndio kwenye maoni huru ya watanzania. Huko mtaani ambako mtu anafahamika ni hatari kuchangia kwa maoni yako kwa uhuru against serikali, kwani unaweza kuhujumiwa eneo lako la kukuingizia kipato.
 
Angalia sasa unazungumzia kuzimwa mitandao 2020 wakati sasa tupo 2022 na mitandao haijafungwa, toa mifano ni jinsi gani hii mitandao inaipa pressure serikali na sio kuniambia kuzimwa mitandao 2020 wakati toka Samia tu aingie madarakani mmepiga sana kelele juu ya maamuzi yake mbalimbali ila hakuna hata kilichomtingisha ndio kwanza alikuwa anawathibitishia kuwa anafuatilia ila anaishia kuwajibu nyodo tu na hakuna pressure yeyote.

Sasa wewe unakuja na habari za mwaka 2020 kitu ambacho hata isingezimwa hiyo mitandao bado isingeleta shida yeyote sana sana kawapa bichwa tu ndio maana umeshikilia hilo hilo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…