Rais Samia awasili jijini Addis Ababa nchini Ethiopia

Rais Samia awasili jijini Addis Ababa nchini Ethiopia

Dunia ni Kijiji saizi,

Hivi hakuna uwezekano kiongozi wetu akafanya nao mikutano kupitia mitandao bila kusafiri Ili kupunguza gharama Kwa wananchi?

Mbona enzi za CORONA mikutano hii ilifanyika?

Balozi anakuwa kule anahakikisha Rais anakuwa hewani, mkutano Unaendelea.

Wananchi wanalala njaa, hawana chakula halafu wanasikia kiongozi wao anasafiri kwenda nje Kwa billions of money za walipakodi!!!
Tunapanua nchi, ndio sera yetu katika hii awamu ya shida
 
Addis Ababa

Thursday, February 16, 2023​

TANZANIA, ANGOLA ZASAINI HATI ZA MAKUBALIANO​


Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola zimesaini Hati mbili za Makubaliano (MoU) kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Ushirikiano kati ya Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania (CFR) na Chuo cha Venancio de Moura cha Angola.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mara baada ya kusaini Hati hizo za Makubaliano, Dkt. Tax alisema Tanzania na Angola zimekuwa zikishirikiana kwa muda mrefu, na Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuzisaidia nchi za Kusini mwa Bara la Afrika kujikomboa na tangu wakati huo imeendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali.

“Leo tumeona ni vyema turasimishe ushirikiano wetu kwa sababu dunia inakwenda mbele na kuna mambo mengi ya kufanya pamoja na hivyo tumesaini Hati mbili za Makubaliano ya kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja itakayotuwezesha kukutana na kujadili masuala mbalimbali yenye manufaa kwa pande zote mbili.
………lakini sisi kwa kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) tutaweza kujadili yanayojiri katika Kanda zetu na Kimataifa na kuona tunavyoweza kufanyia kazi kwa pamoja kwani umoja ni nguvu,” alisema Dkt. Tax

Kuhusu Makubaliano ya Ushirikiano wa Vyuo vya Diplomasia kati ya Tanzania na Angola, Waziri Tax alisema kupitia makubaliano hayo vyuo hivyo vitaweza kubadilishana uzoefu, utaalamu na wanafunzi ili kuboresha taasisi hizo za diplomasia.
“Kupitia makubaliano tuliyosaini leo, vyuo vyetu vya Dioplomasia vitabadilishana uzoefu, utaalamu na wanafunzi ili kuboresha zaidi taasisi zetu hizi za diplomasia,” alisema Waziri Tax.

Kwa Upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António amesema Angola imefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya Tanzania kukubali kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na kuelezea utayari wake wa kushirikiana katika nyanja mbalimbali kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Tanzania na Angola ni marafiki wa siku nyingi, kupiti makubaliano tuliyosaini leo tumefungua ukurasa mpya wa ushirikiano baina ya mataifa yetu, tunayo mengi ya kushirikiana.

Kadhalika, kuhusu ushirikiano wa vyuo vyetu Waangola tumekuwa tukija kujifunza masuala mbalimbali ya kidiplomasia katika Chuo cha Diplomasia (CFR) na kuwa wanadiplomasia, hivyo kupitia makubaliano ya leo tutaweza kubadilishana uzoefu wa kidiplomasia na kuwanoa wanadiplomasia wengi zaidi,” alisema Balozi António.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Balozi Téte António wakisaini Hati za Makubaliano (MoUs) za kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Hati ya Ushirikiano kati ya Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania (CFR) na Chuo cha Venancio de Moura cha Angola. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari 2023
 
17 February 2023
Addis Ababa, Ethiopia

Sisi ni Washindi asema waziri Bi. Naledi Pandor

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa nchi ya Afrika ya Kusini Bi. Naledi Pandor, anyooshea kidole Mabeberu toka nje ya bara Afrika kuwa wanachochea vurugu na mapigano yanayoendelea katika nchi za Afrika, lakini hatimaye bara la Afrika itashinda dhahama hii na kuibuka tumesimama juu kama washindi .

Africa is Standing Up - South Africa’s Minister of International Relations and Cooperation, Naledi Pandor


Source : ENA
 
Back
Top Bottom