Rais Samia awasili Saudi Arabia kushiriki mkutano unaozikutanisha nchi za Afrika na Saudi Arabia kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano

Rais Samia awasili Saudi Arabia kushiriki mkutano unaozikutanisha nchi za Afrika na Saudi Arabia kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania,mama wa shoka,chuma cha reli, jasiri muongoza njia,shujaa wa Afrika,simba wa nyika amewasili salama nchini saudi Arabia ambako atashiriki mkutano unaozikutanisha nchi za Afrika na Saudi Arabia utakao fanyika November 10 mjini Riyadh,unaoangazia kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika sekta za biashara,kilimo,utalii,nishati,uwekezaji na madini.

Ikumbukwe na kueleweka ya kuwa mikutano ya aina hii ni muhimu kwa kuwa inawakutanisha wafanyabishara na wawekezaji wakubwa sana katika Secta hizo tajwa,ambapo ni fursa nzuri kwetu kama Taifa kupata wawekezaji wenye tija na manufaa kwa maslahi mapana ya Taifa letu na ustawi wa watanzania.

Ikumbukwe kuwa fursa zinatafutwa na kila mtu ,hivyo ukikaa tu pasipo kuzitafuta na kuzivutia nchini mwako usifikiri zitakuja tu zenyewe kana kwamba Tanzania tupo pekee yetu au tunavitu vya kipekee ambavyo havipo kwingineko. Ni kupitia fursa hizo ambapo tutatengeneza fursa za ajira kwa vijana, maendeleo ya viwanda,kilimo,utalii, uchumi,kuongeza mapato na kupanua wigo wa kodi.

Hakuna nchi isiyotaka au kuhitaji wawekezaji wakubwa.kila nchi inahitaji wawekezaji na ndio maana tuna ona kila nchi ikijaribu kuweka sera na sheria zitakazovutia wawekezaji wengi ,huku ikilinda na kuhakikishia kuwa wawekezaji wanaokuja ni wenye tija ,kwa kusaini mikataba yenye matokeo chanya yenye kuzingatia maslahi ya Taifa na usalama wake,yenye kuzingatia utamaduni wetu na uwekezaji usio pora uhuru wa Taifa letu lakini ambayo haitaliumiza Taifa wala kuleta maumivu kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho .

Kikubwa watanzania tuendelee kuchangamkia fursa ambazo mh Rais anazileta hapa Nchini.lakini pia serikali yetu ihakikishe ya kuwa kila itakapoweka wino wake kusaini mkataba wa aina yoyote ile basi uwe ni mkataba ambao hata vizazi vijavyo baada ya miaka mingi mbele vikija kuusoma vitikise kichwa kwa Tabasamu na kusema kuwa kwa hakika mkataba huu ulisainiwa na wazalendo wa kweli na wenye upendo na Taifa letu na haya ndio matunda yake.

Serikali ihakikishe kwa kila namna wafanyabiashara wetu hapa nchini wanapata nafasi ya kushirikiana na wawekezaji wa nje ili hata siku wageni wakitaka kuondoka basi tusiteteleke na tubakiwe na ujuzi na maarifa ya namna ya uendeshaji.tuzoe fursa zote popote pale Duniani zenye kulifaidisha Taifa na zile zenye kulinyonya Taifa tuziache na kuzipa kisogo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Sawa kazi iendelee hila usisahau jumamosi pale Nsalaga kunajambo
IMG-20231107-WA0003.jpg
 
Aisee uzi bora kabisa, pokea muamala kijana mzalendo

Umetuma kikamilifu TSh 500,000 kwenda kwa LUCAS MWASHAMBWA Vodacom -255742676627 Jumla ya makato TSh 9675, VAT TSh 1741 Salio jipya ni TSh 509,500. Namba ya muamala: 9743239103814. Risiti: ATY-504382-47373838. 10/11/23 08:05
 
Sawa kazi iendelee hila usisahau jumamosi pale Nsalaga kunajamboView attachment 2809338
Safi sana kwa hakika ni lazima tumpokee Rais wa IPU na mbunge wetu kwa kishindo .kwa hakika ametuheshimisha sana kama Taifa na tuna kila sababu ya kumpongeza kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwa Mbeya na Taifa zima kwa ujumla wake.
 
Kwanini asihamishie ofisi yake huko ili asipate shida ya kusafiri kila mara kwenda huko?

Nadhani ikulu ya Dom tungeijenga Riyadh ama Doha ili mama yetu kipenzi asipate shida ya kupanda ndege kwenda kutafuta fedha za kuwainua Watanzania kiuchumi....

Mama mitano tena jamani, anafanya kazi kubwa sana...
 
Amewasili na fasta kala mkopo kwa hao wajomba.

Arabic ligue wameamua kuingia afrika kwa nguvu mno, hapa wameamua kutoa mikopo mbele kwa mbele, mengine tutajuana baadaye kwenye kudaiana huko!!.
 
Kwanini asihamishie ofisi yake huko ili asipate shida ya kusafiri kila mara kwenda huko?

Nadhani ikulu ya Dom tungeijenga Riyadh ama Doha ili mama yetu kipenzi asipate shida ya kupanda ndege kwenda kutafuta fedha za kuwainua Watanzania kiuchumi....

Mama mitano tena jamani, anafanya kazi kubwa sana...
Tanzania siyo kisiwa ndugu yangu.katika Dunia hii ya ushindani ukibweteka tu lazima uachwe nyuma.ndio maana Rais wetu anapambana usiku na mchana kuhakikisha kuwa Tanzania hatubaki nyuma wala kuachwa nyuma katika Dunia inayokwenda kwa kasi ya mabadiliko.ni lazima tuende na kasi ya Dunia ya kutafuta fursa.
 
Mjinga wewe unasubiri waarabu na wachina wakuletee maendeleo, maendeleo unatakiwa ujiletee mwenyewe. Acha mawazo ya kijinga
Kwa hiyo wewe utanunua pamba,korosho, kahawa,alizeti,mahindi yote n.k? Ili ufaidike na vitu ulivyonavyo ni lazima upate soko lake na ili ulipate ni lazima upate wawekezaji wenye kuja na pesa za kutosha.tujiandae na kuzipokea fursa aziletazo Rais samia.tulime sana,tufuge sana kwakuwa soko ni uhakika chini ya uongozi wa Rais samia.
 
Back
Top Bottom