Rais Samia awasili Saudi Arabia kushiriki mkutano unaozikutanisha nchi za Afrika na Saudi Arabia kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano

Rais Samia awasili Saudi Arabia kushiriki mkutano unaozikutanisha nchi za Afrika na Saudi Arabia kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano

Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania,mama wa shoka,chuma cha reli, jasiri muongoza njia,shujaa wa Afrika,simba wa nyika amewasili salama nchini saudi Arabia ambako atashiriki mkutano unaozikutanisha nchi za Afrika na Saudi Arabia utakao fanyika November 10 mjini Riyadh,unaoangazia kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika sekta za biashara,kilimo,utalii,nishati,uwekezaji na madini.

Ikumbukwe na kueleweka ya kuwa mikutano ya aina hii ni muhimu kwa kuwa inawakutanisha wafanyabishara na wawekezaji wakubwa sana katika Secta hizo tajwa,ambapo ni fursa nzuri kwetu kama Taifa kupata wawekezaji wenye tija na manufaa kwa maslahi mapana ya Taifa letu na ustawi wa watanzania.

Ikumbukwe kuwa fursa zinatafutwa na kila mtu ,hivyo ukikaa tu pasipo kuzitafuta na kuzivutia nchini mwako usifikiri zitakuja tu zenyewe kana kwamba Tanzania tupo pekee yetu au tunavitu vya kipekee ambavyo havipo kwingineko. Ni kupitia fursa hizo ambapo tutatengeneza fursa za ajira kwa vijana, maendeleo ya viwanda,kilimo,utalii, uchumi,kuongeza mapato na kupanua wigo wa kodi.

Hakuna nchi isiyotaka au kuhitaji wawekezaji wakubwa.kila nchi inahitaji wawekezaji na ndio maana tuna ona kila nchi ikijaribu kuweka sera na sheria zitakazovutia wawekezaji wengi ,huku ikilinda na kuhakikishia kuwa wawekezaji wanaokuja ni wenye tija ,kwa kusaini mikataba yenye matokeo chanya yenye kuzingatia maslahi ya Taifa na usalama wake,yenye kuzingatia utamaduni wetu na uwekezaji usio pora uhuru wa Taifa letu lakini ambayo haitaliumiza Taifa wala kuleta maumivu kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho .

Kikubwa watanzania tuendelee kuchangamkia fursa ambazo mh Rais anazileta hapa Nchini.lakini pia serikali yetu ihakikishe ya kuwa kila itakapoweka wino wake kusaini mkataba wa aina yoyote ile basi uwe ni mkataba ambao hata vizazi vijavyo baada ya miaka mingi mbele vikija kuusoma vitikise kichwa kwa Tabasamu na kusema kuwa kwa hakika mkataba huu ulisainiwa na wazalendo wa kweli na wenye upendo na Taifa letu na haya ndio matunda yake.

Serikali ihakikishe kwa kila namna wafanyabiashara wetu hapa nchini wanapata nafasi ya kushirikiana na wawekezaji wa nje ili hata siku wageni wakitaka kuondoka basi tusiteteleke na tubakiwe na ujuzi na maarifa ya namna ya uendeshaji.tuzoe fursa zote popote pale Duniani zenye kulifaidisha Taifa na zile zenye kulinyonya Taifa tuziache na kuzipa kisogo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Kwa hiyo Africa inakutana na Saudi Arabia? Tumerogwa sio bure
 
Atasaini Jambo Lolote Huko Ilimradi Tanzania
Iishiwe
 
Awamu hii ya saudia.....khaawa
Mbona wameenda maraisi wengi tu wa africa including kagame, kuna mkutano mkubwa wa mataifa ya africa na saudi arabia
 
Attachments

  • Screenshot_20231110-080708_Instagram.jpg
    Screenshot_20231110-080708_Instagram.jpg
    72.3 KB · Views: 1
Maendeleo yanaletwa Kwa ushirikiano,ukijifungia na umaskini wako utapata maendeleo yapi Sasa.

Wachina , Waarabu nk ni wawekezaji na Wana mtaji Kwa Kushirikiana nao inakusaidia wewe maskini kujenga uwezo na kujikwamua.

View: https://twitter.com/UchumiForum/status/1722833833404354631?t=rO4cTnN0XUdXPKyLhrEpqA&s=19

Kwani tunashindwa nini sisi kuwezesha wazawa kwa kuwakopesha? mchina anachukua tenda ya barabara 97% ya wafanyakazi ni watanzania yeye kuvuta shisha chini ya mti, mbona serikali inaweza kuwajengea uwezo na wakafanya kazi nzuri
 
Kwa hiyo wewe utanunua pamba,korosho, kahawa,alizeti,mahindi yote n.k? Ili ufaidike na vitu ulivyonavyo ni lazima upate soko lake na ili ulipate ni lazima upate wawekezaji wenye kuja na pesa za kutosha.tujiandae na kuzipokea fursa aziletazo Rais samia.tulime sana,tufuge sana kwakuwa soko ni uhakika chini ya uongozi wa Rais samia.
We ni mjinga, lini umeuza mahindi, mtama, mbaazi Saudi Arabia? East Africa inazaidi ya watu milioni 200 ambapo ni soko tosha
 
Kwani tunashindwa nini sisi kuwezesha wazawa kwa kuwakopesha? mchina anachukua tenda ya barabara 97% ya wafanyakazi ni watanzania yeye kuvuta shisha chini ya mti, mbona serikali inaweza kuwajengea uwezo na wakafanya kazi nzuri
Kwani mtanzania yupi amezuiwa kuwekeza katika sekta yoyote ile hapa nchini? Kwani akina Dewji hawajawekeza? Kwa hiyo unafikiri tukiwa na wawekezaji wachache watasaidia kuzalisha fursa za ajira za kutoshaa? Ni lazima tupate wawekezaji wengi na kuwa na wigo mpana wa kukusanya hata kodi. Lakini pia hata wewe mwenyewe hapo ulipo kama una nafasi na uwezo wa kuwekeza unayo fursa hiyo bila shida tena utapewa kipaombele.
 
We ni mjinga, lini umeuza mahindi, mtama, mbaazi Saudi Arabia? East Africa inazaidi ya watu milioni 200 ambapo ni soko tosha
Hatuuzi nje mahindi bali tunauza unga ili kuchochea viwanda nchini mwetu. Mbaazi tunauza India na ndio maana yakufanya mashirikiano na mataifa mbalimbali nasiyo kujifungia ndani kama panya.
 
Kwani mtanzania yupi amezuiwa kuwekeza katika sekta yoyote ile hapa nchini? Kwani akina Dewji hawajawekeza? Kwa hiyo unafikiri tukiwa na wawekezaji wachache watasaidia kuzalisha fursa za ajira za kutoshaa? Ni lazima tupate wawekezaji wengi na kuwa na wigo mpana wa kukusanya hata kodi. Lakini pia hata wewe mwenyewe hapo ulipo kama una nafasi na uwezo wa kuwekeza unayo fursa hiyo bila shida tena utapewa kipaombele.
Serikali ina wajibu wa kutengeneza mabilionea wazawa na siyo mafisadi ya kuiba mali za umma, serikali inawaweza kuwadhamini/kuwakopesha mitaji wajasiriamali wa kati wakainuka.
 
Hatuuzi nje mahindi bali tunauza unga ili kuchochea viwanda nchini mwetu. Mbaazi tunauza India na ndio maana yakufanya mashirikiano na mataifa mbalimbali nasiyo kujifungia ndani kama panya.
Hapa ndani tu kwenye soko lipo la kutosha, ni aibu leo Tanzania kuagiza ngano na mafuta ya kula Ukraine kwenye nchi ndogo kuliko hata Mkoa wa Singida, sukari tunaagiza nje ni upumbavu mtupu. Soko lipo hapa ndani tena la kutosha
 
Sisi tunatakiwa kuuza nje na siyo kutafuta wawekezaji uchwara, tutatafuta mpaka lini hao wawekezaji? Hapa ndani kuna soko kubwa sn la ngano, sukari, mafuta ya kula sijui matairi ya magari n.k.
Huko nje unakwenda kuuza kwa nani kama huna ushirikiano? Unampelekea nani? Au Unakwenda kichwa kichwa tu kama hayawani?
 
Back
Top Bottom