Rais Samia awatembelea Mzee Makamba, Mama Maria Nyerere pamoja na Familia ya Marehemu Membe leo 14 Julai 2023

Rais Samia awatembelea Mzee Makamba, Mama Maria Nyerere pamoja na Familia ya Marehemu Membe leo 14 Julai 2023

Vipi wale waloitwa polisi wameshaachiliwa huru na kurejea majumbani mwao?
 
Daaah Kweli anasoma mkataba wa bandari kwa misele hii?
Asante
 
Barabara ya kwenda kwa Mzee Makamba ilichorongwa jana usiku ile mheshimiwa apite, hii barabara haijaliona greda miaka, ni barabara ya kutoka Kondoa Wazo Tegeta kwenda Kisanga kupitia kanisa la RC hadi nyumbani kwa mheshimiwa sana Makamba, watu wamejiuliza kwani sasa ndio pesa wameitoa wapi kwani tuliambiwa hakuna hela, pia naona hii ziara ni ya kushtukiza ndio maana greda imechoronga hii barabara usiku kama saa tatu hivi. Tunashukuru ujio wa mama angalau bajaji sasa zitapita bila kuingia mashimoni.
 
Kwa nyakati tofauti leo Julai 14 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea na kumfariji Mama Dorcas Membe Mjane wa Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Hayati Bernard Membe nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Rais Samia pia amemtembelea Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mzee Yusuf Makamba nyumbani kwake Wazo Jijini Dar es Salaam.

Vilevile Rais Samia amemtembelea kumsalimia na kumjulia hali Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam.

View attachment 2688103
View attachment 2688104
View attachment 2688105
View attachment 2688106
View attachment 2688107
Amenda kutoa stress za dp world
 
Kaenda kuomba msamaha kwa mjane wa muasisi wa Taifa.
 
Ulichokiona ni nini hadi umpe daraja la upendo na kuheshimu utu.

sijawahi kukutana na Rais lakini ninapo muona kila mahali anapo kwenda ni mtu mwenye kuheshimu sana binadaamu wenzake awe mdogo au mkubwa, kwake yeye Urais haujamvaa bali kauvaa Urais.

viongozi wengine wanapaswa kumuiga sana Rais sio mtu wa kujivuna wala kujisikia yeye ni Rais kiongozi wa juu zaidi lakini ....yuko simple na humble kwa kila mtu......
 
Daah, hatari, ila..

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

Tanganyika wazanzibar wanachukua Mali yetu kisa Cha muwekezaji jamani.
WHY WHY BANDARI ZA ZANZIBAR No. KUWA FAIDA WACHUKUE WAO TU YOTE HATA TANGANYIKA ISIPATE FAIDA YA 0TZS. HUKU MASIKINI WAKIUMIZWA NA KODI YA MIAMALA NA KILA SEHEMU IMEJAA KODI WHY HUYO ASEMEHEWE KODI HAMUONI KUWA HAO JAMAA WANAJILIPA KWENYE BANDARI KAMA WENGINE WALIVYOKWISHAJILIPA KWENYE UMEME, GESI NA MAFUTA WAO TU NDIO MADILA BASI PAMOJA NA SUKARI.

WATU MMELALA SIJUI MTAJUJA KUWAAMBIAJE WAJUKUU ZENU WATAKAPOKUWA HAWANA PA KWENDA NA KUTUMIKISHWA KAMA PUNDA NA HUKU WEWE UMESHIBA LEO PEKEE.

JAMANI ACHENI UOGA KIZAZI CHA AKINA NYERERE WALITESEKA SIE TUWE HURU WHY SIE TUNAKUWA WAOGA NA ASKARI ANAGANYA KAZI KAMA ROBOTI ANAUA MTU ANAYETETEA TAIFA KISA CHA AJIRA YAKE AMBAYO KWANZA INAMFANYA AWE MASIKINI.
ANGALIENI NCHI YETU IMESHAUZWA IMEISHA PORI TENGEFU, MADINI YAMEISHA YOTE WANAWAPA WATU KWA GAWIO LA SIRI KIVYAO NA SIO LA SERIKALI.

BAADAYE UNAKAMULIWA KODI MPAKA VIMA YAISHE.


YAANI HUJIULIZI UNALIPWA SALARY KODI, UKITOA HELA BANK KODI, UKIITUMA KODI, UKIITOA ULIYOTUMIWA KODI, UKINUNUA KITU KODI , YAANI KUNA KODI NYINGI MNO UNALIWA MPAKA UNAKUJA KUIPATA HELA YAKO.
HUKU WATU WAKIWAPA MA EX WAO GARI ZA 500M.
Peleka kwa lissu, slaa na mbowe wakupatie majibu. Mama is too busy kutekeleza shughuli za maendeleo wajinga nyie!!
 
Kwa nyakati tofauti leo Julai 14 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea na kumfariji Mama Dorcas Membe Mjane wa Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Hayati Bernard Membe nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Rais Samia pia amemtembelea Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mzee Yusuf Makamba nyumbani kwake Wazo Jijini Dar es Salaam.

Vilevile Rais Samia amemtembelea kumsalimia na kumjulia hali Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam.

View attachment 2688103
View attachment 2688104
View attachment 2688105
View attachment 2688106
View attachment 2688107
Mzee wa kutoshirikisha hekima kwenye mtamko yake anaingia kukinukisha soon.

Subirini Watanzania tunaohoji tutakavyosutwa na kutukanwa.

Mama anapaswa kuvunja Baraza la Mawaziri hajachelewa bado.
 
Back
Top Bottom