Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa njiani kutoka Mwanza kwenda mkoani Mara, leo Ijumaa ametangaza kutengua uteuzi wa wakurugenzi wanne wa Halmashauri ya Buchosha, Iringa, Mbeya na Singida Mjini baada ya kubainika kutumia vibaya fedha za UVIKO-19.
---
Your browser is not able to display this video.
Rais Samia Suluhu Hassan amewatengua Wakurugenzi wa Halmashauri nne kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na amesema Mkurugenzi wa Geita kama akikutwa na ubadhirifu pia tataenguliwa
Wakurugenzi waliotenguliwa ni Mkurugenzi wa Buchosa, Iringa, Mbeya Mjini na Singida Mjini. Utenguzi umefanyika baada ya Waziri wa OR-TAMISEMI Innocent Bashungwa kusema wanafanya uchunguzi wa haraka kwa wakurugenzi walioripotiwa kufanya ubadhirifu
Halmashauri ya Buchosa ilikuwa chini ya Mkurugenzi Paulo Malala, Mkurugenzi wa Iringa ni Limbe B. Limbe, Mkurugenzi wa Singida Mjini ni Zefrin Kimolo Lubuva, na Mbeya Mjini ni Amede E.A Ngwanidako
Rais Samia Suluhu Hassan amewatengua Wakurugenzi wa Halmashauri nne kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na amesema Mkurugenzi wa Geita kama akikutwa na ubadhirifu pia tataenguliwa
Wakurugenzi waliotenguliwa ni Mkurugenzi wa Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini. Utenguzi umefanyika baada ya Waziri wa OR-TAMISEMI Innocent Bashungwa kusema wanafanya uchunguzi wa haraka kwa wakurugenzi walioripotiwa kufanya ubadhirifu.
Halmashauri ya Buchosa ilikuwa chini ya Mkurugenzi Paulo Malala, Mkurugenzi wa Iringa ni Limbe B. Limbe, Mkurugenzi wa Singida Mjini ni Zefrin Kimolo Lubuva, na Mbeya
Mama Samia amewatengua wakurugenzi wanne wa halmashauri za Buchosa, singida mjini, Itinga na Mbeya kwa matumizi mabaya ya pesa za Uviko.
Mama Samia nakuunga mkono kwa 100%, kwa kuwa hizi pesa watakaokuja kuzilipa ni wananchi hivyo zinapaswa kutumiwa vizuri ili kuleta maendeleo.
Mfuko wa cement unauzwa 21000 lakini mkurugenzi anaenda kununua kwa 24000. Haya ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi na n Bora umeliona hili, japo hapo mwanzo walikuwepo washabiki wakawa wanatetea humu sijui Leo watasemaje.
Mama Samia endelea kuhakikisha kila pesa ya serikali kwenye miradi haipotei.
Lakini pia usiishie kuwatengua tu unaweza kwenda mbali kwa kuwawajibisha zaidi ili kuzuia wengine kujipimia kwa urefu wa kamba zao.
Hao kosa lao itakuwa wamekula wakavimbiwa, Rais hapendi hilo anataka ule kwa kiasi.
Huyo mkurugenzi wa Iringa sio yule alieshutumiwa kwa ubakaji siku chache zilizopita? kama ndie akapumzike tu, yeye alikuwa hachagui vyakula anabugia chochote.
Rais Samia Suluhu Hassan amewatengua Wakurugenzi wa Halmashauri nne kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na amesema Mkurugenzi wa Geita kama akikutwa na ubadhirifu pia tataenguliwa....
... huyu Limbe si ndiye kulikuwa na uzi humu unamhusu kwamba alimuita baa mdada mmoja aliyekuwa na shida ya kiofisi akamlewesha na hatimaye kwenda kumbaka gesti? Jinga sana hili wamelichelewesha sana!