Rais Samia awatumbua Wakurugenzi wa Halmashauri wanne kwa ubadhirifu wa Fedha zikiwemo za UVIKO-19

Rais Samia awatumbua Wakurugenzi wa Halmashauri wanne kwa ubadhirifu wa Fedha zikiwemo za UVIKO-19

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa njiani kutoka Mwanza kwenda mkoani Mara, leo Ijumaa ametangaza kutengua uteuzi wa wakurugenzi wanne wa Halmashauri ya Buchosha, Iringa, Mbeya na Singida Mjini baada ya kubainika kutumia vibaya fedha za UVIKO-19.

---
Ni ng'wanidako
 
... huyu Limbe si ndiye kulikuwa na uzi humu unamhusu kwamba alimuita baa mdada mmoja aliyekuwa na shida ya kiofisi akamlewesha na hatimaye kwenda kumbaka gesti? Jinga sana hili wamelichelewesha sana!
Kampa bia za kumwaga na mikuku ya kukaanga kwa pesa za ujenzi wa madarasa. Kamla dada wawatu kavu, limbe huna maana
 
Hivi hao wanaoitwa wabadhirifu, mbona huwa hawafikishwi mahakamani?
 
Hongera sana Rais wetu mpedwa mama Samia, kwa kusimamia weledi na uwajibikaji kwa wateule wako. Hatua uliyochukua itaongeza weledi na nidhamu kwa wateule wako katika kusimamia matumizi ya fedha za umma.
 
si tulikubaliana mpaka zifike Mara 4 ndio tuwatumbue wale wanaokosea ?
Kuiba na kukosea ni vitu viwili tofauti.. Naendelea kusisitiza kula kwa urefu wa kamba yako ukizidisha utaliwa kichwa..

Mh.Rais naomba usiishie kwenye kutumbua tuu bali wafikishwe kizimbani ,pia iwe hivyo kwenye pesa zote za umma sio za Uviko 19 tuu.
 
Kama wameiba tusiishie tu kuwatumbua bali jela pia ni muhimu, wafirisiwe kufidia ujinga wao... wapelekwe mahakamani kwa kosa la uhujumu uchumi na mengine....Itakuwa ujumbe mzuri kwa wengine na wapumbavu wote...
 
Huyu wa Iringa si alikula tunda kimasihara kwa mtumishi wake iliwahi ripotiwa humu alikuwa anafuatialia BIMA kesi hiyo ya kubaka.
 
Lipo wazi report ya CAG ikija huko kwenye wilaya kumejaa hati chafu ndio sababu ya kumtoa shosti wake na kumpeleka afya lawama abebe mwingine.
 
Bashungwa hicho Cha leo wahehe wanaita ni kimulimuli ,kaza buti tamisemi mama Kisha kwambia na mtindo wa kufichaficha waovu,na hao ni sehemu ya genge kubwa la wezi waliovaa majoho ya tumeteuliwa na Raisi.
 
Hadi sasa wakurugenzi matumbo joto. Hii fedha ya ujenzi wa madarasa imepigwa sana. Mama Samia Rais wa JMT usikubali kamba ya kitanzi wafe nayo wakurugenzi tuu. Tengua maafisa elimu na wakuu wa shule wenye izo tuhuma na walipe fedha kwa makosaya uhujumu uchumi. Wana JF tutupie majengo yaliojengwa chini ya kiwango. Tuwatag na tuwaabishe. Huko buchosa kuna shule majengo mapya yamechomwa moto ili kuficha ufisadi uliofanyika. Ushaidi tunao
 

RAIS SAMIA SULUHU ATUMBUA WAKURUGENZI WANNE WA HALMASHAURI...AMUWEKA KIPORO YULE WA GEITA,​


AVvXsEj2-phnDfnSWUHW5aHR4ta6-8f4tD0rkV2Y5qRet-cmnEofFsTAkFX3KYWbYn0Eo-nGuAuAyakQoFbIeP3oVxAQmyTqH3areMYcl0i19CRit018xGILSTQXYv_KwqkaxDFqAt4Xt_MD7hGXMKG8QwrxgxDqW1k_xndodvjnCAxpNlzCBuw_FHcclUXasQ=w640-h432

======
RAIS Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Februari 4, 2022 akiwa njiani Magu jijini Mwanza akielekea Musoma mkoani Mara,

Rais Samia ametengua uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini,

Wakurugenzi hawa wanakabiliwa kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo na upotevu wa mapato katika halmashauri zao,

“Siku ile tunazitangaza fedha nilisema kama mkurugenzi anataka kuona rangi yangu halisi achezee hizo fedha "

Rais Samia Suluhu amesema traarifa zilizopo, Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini, wakurugenzi wamechezea fedha.

" Mheshimiwa waziri (Waziri wa Tamisemi) wakurugenzi hao nimewatengua sasa hivi” amesema Rais Samia na kuongeza

“Yule wa Geita endeleeni na uchunguzi, na mimi timu yangu iko pale inafanya uchunguzi naye wakiniletea na makossa kama haya nay eye attatenguliwa” amesema

Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa alisema kuwa Wizara hiyo ilipata taarifa za ubadhirifu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kuhusu Wilaya ya Buchosa na maeneo mengine.

Waziri Bashungwa alianza kwa kutoa pongezi kwa Rais Samia kutokana na ujenzi wa madarasa ya fedha za Uviko-19.

Baada ya kumaliza, Rais Samia alimuagiza Waziri Bashungwa kutaja maeneo mengine ambayo kumefanyika ubadhirifu.
 
Back
Top Bottom