Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi wengine wakati akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Bandari za Ziwa Tanganyika (Kibirizi na Ujiji) katika Sherehe zilizofanyika Kibirizi Mkoani Kigoma, Oktoba 18, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi wengine wakati walipotembelea eneo la Bandari ya Kibirizi katika Ziwa Tanganyika mara baada ya kuweka jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Bandari za Ziwa Tanganyika katika Sherehe zilizofanyika Kigoma Mjini, Oktoba 18, 2022.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Prasduce Mbossa akitoa maelezo ya mradi wa Kibirizi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan mara baada ya Mhe. Rais kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bandari za Kibirizi na Ujiji pamoja na Jengo la Utawala mjini Kigoma, Oktoba 18, 2022.