Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Aidha, Rais amezindua maeneo manne ya mradi huo ambayo ni; Njia ya umeme msongo wa Kilovoti 220 kutoka Geita mpaka Nyakanazi yenye urefu wa Kilomita 144, Kituo cha Kupoza umeme cha Nyakanazi kutoka kilovoti 220 mpaka kilovoti 33 na matoleo yake sita, Njia ya kwanza inayopeleka umeme wa Gridi ya Taifa Mkoani Kigoma kupitia Kibondo hadi Kasulu na Njia ya kupokea umeme mkubwa wa Kilovoti 220 kutoka Rusumo yenye urefu wa Kilomita 94.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Nishati, January Makamba pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuzindua miradi sita ya umeme, ikiwemo Njia ya kusafirisha umeme wa msongo Kv 220 kutoka Nyakanazi -Geita, Nyakanazi Rusumo, Kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Nyakanazi pamoja na njia kubwa za kusafirisha umeme kwenda Mkoa wa Kigoma tarehe 16 Oktoba, 2022 Mkoani Kagera.
Kukamilika kwa mradi huo kunafanya maeneo ya Chato, Biharamuro na Ngara ambayo yalikuwa yanapata umeme mdogo na kutumia jenereta, sasa yanaanza kupata umeme wa uhakika
Pia, Shirika la Umeme Tazania (TANESCO) limesema mradi huo utawafanya wazime jenereta za Biharamuro, Ngara, Kibondo na Kasulu, hivyo kuokoa gharama za mafuta na matengenezo zaidi ya Tsh. bilioni 60.
Imeelezwa mradi utasaidia usalama kwa kupokea umeme kutoka kituo cha kufua umeme cha Rusumo kitakapokamilika 2021 na kupeleka umeme wa Gridi ya Taifa Bukoba kupitia Benaco hadi Kyaka na migodi ya Kabanga.
Pamoja na uzinduzi huu, Rais Samia ameweka jiwe la msingi wa kituo cha kukuza umeme cha Nyakanazi kutoka kilovoti 220 hadi Kilovoti 440 pamoja na njia kubwa ya umeme wa msongo wa Kilovoti 400 yenye urefu wa Kilomita 280 ya kutoka Nyakanazi hadi Kigoma.
Taarifa ya TANESCO imeeleza kuwa mradi huu ukikamilika mwishoni mwa 2023 utanufaisha Mkoa wa Kigoma na kufungua fursa ya kusafirisha umeme kwenda nchi jirani.
Miradi yote hii inagharimu takriban Tsh. Bilioni 600 na inagharimiwa na Serikali ya Tanzania na fedha za mikopo kutoka kwa African Developement Bank (AfDB), Agence Francaise de Development (AFD) pamoja na Korea Economic Development Co-operation (EDCF).