Rais Samia azindua ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani kilimo. Asema Serikali imeongeza bajeti ya utafiti kutoka Tsh 7.35bn hadi 11bn

Ni utaratibu mzuri kwa wakulima watakao kuwa serious, hii itasaidia commercial farms nyingi kuanzishwa maana capital is everything kwenye hizi farms, lakini sheria za ardhi na serikali kuingilia ingilia wakulima especially kwenye bei na mauzo ya mavuno yao inaweza kuwa issue, kazi bado anayo kama anataka mapinduzi ya kweli lakini mwanzo mzuri
 
Msoga wasipomzonga naona ni mmoja wa vijana wenye nia njema na nchi hii...anajua anachokifanya... hongera kwa JPM kuibua kipaji.
Bashe hajaibuliwa na marehemu wenu tafuteni sehemu nyingine ya kujiliwaza.

Bashe anajurikana kitambo kama yuko vizuri upstairs, labda umtaje Rostam Aziz ndiye aliyemuibuwa unaweza kueleweka, lakini kwakuwa upo kundi lile la washamba huwezi kulijuwa hili.
 
Hizo Ni porojo tu,wapi kilimo kwanza enzi za jk
 
Ni kamarada H.Bashe tena....

Bashe anaweza....

Bashe is a visionary leader....
Bashe is a charismatic leader.....

TUNATEGEMEA mengi kutoka kwake ,amin🙏

#Siempre JMT🙏
Tatizo kukifanyika mabadiriko usishangae mtu kama huyo kusikia kahamishiwa Tamisemi, ndio shida ya siasa zetu.
 
Nani kama Mama
Hongera Mama na Bashe

Mkirudisha na ruzuku na kujazia nguvu umwagiliaji throughout the year tutashinda

Masoko pia yatafutwe
 
Tatizo mfumo wa ruzuku unahujumiwa kwa viwango vya kutisha
 
Bashe is good.Ila nashauri kwa mara nyingine tena yafuatayo:
1.Maafisa Ugani wawe na weledi unaotakiwa.Wengi wanaogopa kwenda kwa wakulima because they are incompetent.
2.Ihakikishwe kwamba vyombo vyao vya usafiri vipo up and running wakati wote.Kwa hiyo wapewe posho ya mafuta na service inayo tosheleza haja.
3.Hela ya kutosha kwa ajili ya mashamba darasa ijumlishe pia vifaa kama pesticides,sprayers,mbolea nk.
4.Hizo pikipiki baada ya miaka miwili,wapewe ziwe zao,ila waendelee kupata posho ya mafuta na service,in that way watazitunza.Wasainishwe mkataba unaoainisha hili.
5.Nashauri mishahara yao iongezwe,ili kushawizi brains kuingia huko.
6.Mwisho nashauri pia vijana waliofaulu vizuri ndio wachaguliwe ku-pursue course ya Kilimo.

Otherwise hongera sana Bashe,viatu vimekutosha.
 
Daa, haki ya nani, sasa mkuu samia anahusikaje hapo wakati hata huyo bashe ni zao la Magu?
Weee Magu alimzaa Bashe au sio? Kwa hiyo Bashe alikuwa minister wa kilimo enzi za mwendazake au sio?

Kwa akili yako mbovu,Baraza la Mawaziri la Samia na Mwendazake lipi unaona linakuja na majibu ya kero za Wananchi?

Mtwana akifanya vizuri sifa ni za mfalme.

Ukweli unaujua ila chuki zinakuhangaisha.

Hakunaga Rais mtaalamu wa kilimo,injinia,mwanasheria, IGP nk kama yule mjinga alivyowaaminisha wapuuzi kama wewe.
 
Labda mapinduzi ya Kilimo CHUMBANI KWAKE
 
Labda mapinduzi ya Kilimo CHUMBANI KWAKE huko.

Hakuna nchi yoyote ile Duniani iliyowahi kufanya Mapinduzi ya Kilimo kwa Bajeti ya $ 40M. Hizo fedha ni Sawa na Bajeti ya Shule ya Msingi hapo SOUTH AFRICA TU.
 
Labda mapinduzi ya Kilimo CHUMBANI KWAKE huko.

Hakuna nchi yoyote ile Duniani iliyowahi kufanya Mapinduzi ya Kilimo kwa Bajeti ya $ 40M. Hizo fedha ni Sawa na Bajeti ya Shule ya Msingi hapo SOUTH AFRICA TU.
Shule ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…