Rais Samia, Bado hujaona hili ni tatizo tu?

Rais Samia, Bado hujaona hili ni tatizo tu?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Ukimsikiliza Ndugai wa leo sio yule wa miezi miwli nyuma kipindi Mama Samia anashika madaraka, huyu wa sasa amerejea kwenye jeuri na kejeri zilezile za utawala wa Magufuli, Anauhakika na anakokwenda. Ukimsikiliza Mwigulu wa sasa, sio yule wa mwanzo wa utawala wa Mama Samia, Mwigulu wa sasa ana jeuri, kibri na dharau iliyovuka mipaka ya siasa za Dar es Salaamu.

Sasa mwangalie na msikilize mpiga filimbi mdini na mkabila aliyekubuhu wa utawala uliopita bwana Josephat Gwajima, huyu si kwamba anampinga tu Rais Mama Samia, Bali amevuka mipaka na kumtuhumu Rais wa nchi kwamba kahongwa pesa na Marekani ili Marekani iuze chanjo nchini. Genge la utawala uliopita wanaamini Samia ni rais wa Mpito sio rais wa "Awamu". Wanaamini rais wa mpito anakoma 2025 na kwamba mipango yao ya kuwania urais haitaharibiwa na urais wa mpito wa Samia.

Awali kabisa tulionya tukitaka Rais mpya Mama Samia aunde serikali yake badala ya kuendeleza serikali ya mtangulizi wake ambayo ilijengwa mfumo hatari na wa kiharamia kwa miaka zaidi ya mtano. Mfumo huo huwezi kuubomboa kwa kubadili mtu mmoja ambae ni rais tu, bali kuivunja serikali nzima na kuunda serikali mpya.

Kwakuwa siasa ya Dar es Salaam ambako kuibuka kwa nguvu na mtu na kuanguka ni jambo lisiloshangaza, Mfumo uliounda serikali iliyopita bado unanguvu kubwa sana ya kimaamuzi, Pengine lilikuwa kosa kubwa sana la karne kwa Mama Samia kuamua kuendesha nchi kwakutumia mfumo wa serikali iliyopita, Huenda ilikuwa kwa nia njema ama kosa la kimahesabu, kwasasa ni vigumu kujinasua, kinyume chake unajikuta umezungwa na ma spinning doctors hata kama una mamlaka kikatiba lakini wenzio wanakukamata kisiasa, michezo kama blackmails ndio inayouteka utawala mpya. Kundi la wahafidhina limefanikiwa kubaki kwenye mfumo,

Juhudi za Rais wa nchi kupambana na corona kwakufuata masharti ya Shirika la Afya dunia, sasa zinapingwa waziwazi na kundi la utawala uliopita ambalo msimamo wao juu ya janga la corona ulikuwa ni wa kijadi zaidi hali iliyopelekea watu wengi kupoteza maisha katika nchi. Kuhusu Chanjo kwa Tanzania inatakiwa serikali isimame wima itoe elimu ya haraka na ya lazima umuhimu na usalama wa chanjo husika.

Jamii iliharibiwa vibaya sana na Rais Magufuli alipotangaza hadharani kuwa chanjo ya corona haifai, Wazungu hawawapendi Watanzania na tuhuma nyingi lukuki, Leo jamii inamwamini Magufuli kuhusu chanjo, sifiriki kwamba Watz wengi watajitokeza kuchanjwa. Badala ya serikali kutangaza tu kuleteta chanjo, iingie mtaani kutoa elimu na kuhamasisha watu wakachanjwa haraka iwezekanavyo.

Mama Samia, vita vya ndani yako ni vikubwa kuliko hivi vya nje ulivyovianzisha, Wenzio wanakusakizia upigane na wapinzani nje huku wanakumaliza ndani, Ya Joyce Banda yanakugonja. Patana na wapinzani ili ushinde vita vyako vya ndani kirahisi. Vita vya nje hutapigana na Chadema tu, utapigana na dunia nzima hata wanaofadhili bajeti yako watakupiga pia na HAUTASHINDA, wewe ni shahidi wa namna Magufuli alivyopitishwa katika magumu alipoamua kutaka kuua upinzani nchini, hakupigana na Chadema tu, alipigana na dunia nzima akaliumiza taifa na akashindwa yeye. Chadema ipo na itaendelea kuwepo.

Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi, inakuwaje mtu kama GWAJIMA anamtuhumu RAIS @SuluhuSamia kuhongwa PESA na Marekani ili kupigia CHAPUO Chanjo ya COVIDE19? Mko busy kuhujumu vyama vya upinzani na kumbambikia kesi ya Ugaidi @freemanmbowetz na kuacha huyu anayehatarisha usalama wa nchi?

Tatizo kubwa katika nchi hii ni kwamba sayansi inageuzwa kuwa siasa. Hakuna jamii iliyowahi kuendelea kwa kubeza sayansi na maarifa. Hakuna sababu ya kugomea chanjo huku ukiendelea kufa, lakini ieleweke kwamba chanjo zote duniani hata za watoto chini ya miaka 5 zina madhara. Kuna wengine hupata hadi vilema lakini tunaendelea kupeleka watoto clinic kwani tunaamini kwamba madhara kama yako chini ya asilimia 0.01 sio shida sana. Pili hawa vurusi wa Covid kwamjibu wa wataalamu wamagonjwa na tiba wanasema vinabadilika- mutate. Hivyo chanjo zinaendelea kuboreshwa kadri wanavyobadilika.

Tuheshimu sayansi na tusikilize wataalamu wanachosema na tuheshimu taalama za wenzetu, tusisikilize wanasiasa na matapeli wa kiroho aina ya Gwajima.

Katika wote hapo uliowataja, sioni hata mmoja mwenye haiba ya kumbabaisha Samia. Apende tu yeye mwenyewe kujiweka katika hali hiyo kwa kukosa ujasiri na uwezo wa kuwa kiongozi.

Gwajima? Ana kitu gani huyo kichwani ni mtupu kabisa! Mama atishike na wafuasi wake huko kanisani?

Gwajima anao msingi upi ndani ya CCM, hata hii mbovu tunayoishuhudia kwamba watajipanga nyuma yake kupambana na mama!

Kelele nyingi tu zisizo na msingi ndizo zimtishe mama?

Ndugai na mwenzake Madilu, sina hata muda wa kupoteza kuwajadili hapa. Hawa ni watu wasiokuwa na nyuma wala mbele, wanayumbayumba tu.

Samia atayumbishwa kwa udhaifu wake mkubwa anaouonyesha waziwazi, hata hawa wapuuzi wanaanza kumchezea.
 
Ni kweli kabisa, alifanya kosa la kiufundi kutovunja serikali aunde yake. Wengi tulitarajia hilo. Alidhani urais alioupata alipewa fadhila ilhali alipigiwa kura na alipiga kampeni sana nchi nzima kuliko hata magufuli.

kwa kadri ambavyo anamuona Mbowe na Chadema ni tishio kwake ndiyo ambavyo hawa vijana wakabila na wadini walikubuhu watakavyoendelea kumtia vidole vya macho.

Na hajashtuka kwamba kuendelea kuwashambulia wapinzani anadhani polisi wanamsaidia, somebody tell her that it is a subotage. Chuki kubwa inaanza kujengeka katika jamii dhidi yake.

Na sasa amekaa kimya polisi kustorm kanisani, jambo ambalo hata jpm hakuwahi kuruhusu likafanyika ijapokuwa aliwaharass sana wapinzani.

Time is a good judge
 
Katika wote hapo uliowataja, sioni hata mmoja mwenye haiba ya kumbabaisha Samia. Apende tu yeye mwenyewe kujiweka katika hali hiyo kwa kukosa ujasiri na uwezo wa kuwa kiongozi.

Gwajima? Ana kitu gani huyo kichwani ni mtupu kabisa! Mama atishike na wafuasi wake huko kanisani?

Gwajima anao msingi upi ndani ya CCM, hata hii mbovu tunayoishuhudia kwamba watajipanga nyuma yake kupambana na mama!

Kelele nyingi tu zisizo na msingi ndizo zimtishe mama?

Ndugai na mwenzake Madilu, sina hata muda wa kupoteza kuwajadili hapa. Hawa ni watu wasiokuwa na nyuma wala mbele, wanayumbayumba tu.

Samia atayumbishwa kwa udhaifu wake mkubwa anaouonyesha waziwazi, hata hawa wapuuzi wanaanza kumchezea.
safi sana, umesummerize alichomaanisha mtoa post, japo umemkosoa. Ni kweli Samia should act now na kwa kishindo. Asiendelee kuwaonea huruma au kuwaogopa hawa washe.nzi. Watamsumbua sana.

The first reaction is always the correct one.
 
Katika wote hapo uliowataja, sioni hata mmoja mwenye haiba ya kumbabaisha Samia. Apende tu yeye mwenyewe kujiweka katika hali hiyo kwa kukosa ujasiri na uwezo wa kuwa kiongozi.

Gwajima? Ana kitu gani huyo kichwani ni mtupu kabisa! Mama atishike na wafuasi wake huko kanisani?

Gwajima anao msingi upi ndani ya CCM, hata hii mbovu tunayoishuhudia kwamba watajipanga nyuma yake kupambana na mama!

Kelele nyingi tu zisizo na msingi ndizo zimtishe mama?

Ndugai na mwenzake Madilu, sina hata muda wa kupoteza kuwajadili hapa. Hawa ni watu wasiokuwa na nyuma wala mbele, wanayumbayumba tu.

Samia atayumbishwa kwa udhaifu wake mkubwa anaouonyesha waziwazi, hata hawa wapuuzi wanaanza kumchezea.
Ayubu alikua spika wa redio Chato, anajua siri nyingi za ndani na ndiyo anapata kiburi cha kumuonyesha madam kuwa hambabaishi.
 
Usemacho ni kweli mtu kawekwa Kati,ukiacha hao wengine nilimsikia Karibu mkuu wizara ya Afya akiongelea hatua za kuchukua ila kwenye chanjo aliongea as if sio kitu cha muhimu .

Nadhani Rais hajachelewa Sana Felix Chisekedi alivunja Ushawishi wa Kabila baada ya miaka 2 ,Mama arudi haraka kwa JK amsaidie kusuka system yake kuanzia kwenye usalama,ndani ya chama,Serikalini afu kwa Wananchi kutaji set kwenyewe.
 
Kuna Maswali mengi ya kujiuliza kuhusu hiyo chanjo, hayajawahi kupatiwa majibu fasaha. Mbona nchi zilizochanjwa ndo zinaongoza kwa maambukizi na vifo? Mbona nchi zilizochanjwa still wanavaa barakoa na kuchukua tahadhari kama kawaida?

Kwanni hizo chanjo zimeonesha kuwa na athari kwa baadhi ya watu waliochoma. Halafu unasema tuheshimu utaalamu wa wenzetu na sayansi wakati so far hazijaonesha matokeo yoyote chanya na ugonjwa bado unaendelea kuitesa dunia.

Hatua zilizochukuliwa na nchi yetu zimeonekana kuwa bora zaidi ikiwemo dawa zetu asilia kuliko hizo za wazungu mnazozitaka. Kwanini tusijivunie vya kwetu tunaendekeza kusifia vya wenzetu. Kwanini mzungu anapinga kujifukiza anataka tutumie chanjo ambazo mpaka sasa hazijaproove kumsaidia yoyote.
 
Ni kweli kabisa, alifanya kosa la kiufundi kutofunja serikali aunde yake. Wengi tulitarajia hilo. Alidhani urais alioupata alipewa fadhila ilhali alipigiwa kura na alipiga kampeni sana nchi nzima kuliko hata magufuli.

kwa kadri ambavyo anamuona Mbowe na Chadema ni tishio kwake ndiyo ambavyo hawa vijana wakabila na wadini walikubuhu watakavyoendelea kumtia vidole vya macho.

Na hajashtuka kwamba kuendelea kuwashambulia wapinzani anadhani polisi na wanamsaidia, somebody tell her that it is a subotage. Chuki kubwa inaanza kujengeka katika jamii dhidi yake.

Na sasa amekaa kimya polisi kustorm kanisani, jambo ambalo hata jpm hakuwahi kuruhusu likafanyika ijapokuwa aliwaharss sana wapinzani.

Time is a good judge
Bora hata VP,PM mwenyewe ni kama kaisusa Serikali...mama fukuza Hawa watu kwanza imefika mahala hata makusanyo ya serikali hawashughuliki kuhimiza kama mwanzo,watu wanaiba dawa za serikali hazifiki za kutosha kwenye vituo vya kutolea huduma nk ..Sasa Wana msaada gani hawa
 
Kuna Maswali mengi ya kujiuliza kuhusu hiyo chanjo, hayajawahi kupatiwa majibu fasaha. Mbona nchi zilizochanjwa ndo zinaongoza kwa maambukizi na vifo? Mbona nchi zilizochanjwa still wanavaa barakoa na kuchukua tahadhari kama kawaida? Kwanni hizo chanjo zimeonesha kuwa na athari kwa baadhi ya watu waliochoma. Halafu unasema tuheshimu utaalamu wa wenzetu na sayansi wakati so far hazijaonesha matokeo yoyote chanya na ugonjwa bado unaendelea kuitesa dunia.

Hatua zilizochukuliwa na nchi yetu zimeonekana kuwa bora zaidi ikiwemo dawa zetu asilia kuliko hizo za wazungu mnazozitaka. Kwanini tusijivunie vya kwetu tunaendekeza kusifia vya wenzetu. Kwanini mzungu anapinga kujifukiza anataka tutumie chanjo ambazo mpaka sasa hazijaproove kumsaidia yoyote.
Na wewe uwe na akili ,Chanjo sio tiba 100 % bali ina boost kiasi fulani cha Kinga hakuna waliposema ukipata chanjo 2 huugui bali chance ya kuugua unaipunguza.

Ndio maana huko unakosema hivyo vifo sio vingi miongoni mwa waliochanjwa na hili sio tuu kwenye chanjo ya Covid 19 hata chanjo zingine kama surua nk.

Kwa uelewa wangu sidhani kama mzungu anapinga kujifukiza nachojua mimi kujifukiza kunakuongezea hatari ya kufa kuliko tiba,kama unaamini hivyo uliza daktari yeyote unaemjua wewe atakupa jibu.Kwa hiyo wakipinga wako sahihi maana ushahidi wa kisayansi haujathibitisha popote japo kwa asilimia chache kwamba kujifukiza ni Kinga au dawa.Kwa hiyo acceptable standards ni chanjo Ili usiwe muenezaji.

Ishu ya kuchukua tahadhari zote iko pale pale maana hakuna mahali ilitangazwa kwenye nchi hizo kwamba mlipuko umekwisha na umedhibitiwa isipokuwa prevelance yake ulipungua but unfortunately mutation ya kirusi bado inaendelea.
 
Kosa Kubwa Ni vile Mama alicopy wale wale watu ambao waliumiza sana Wananchi wenzao...wengine anawajua kwa karibu zaidi hivi kweli Mh Rais Hujui Ubaya wa Joseph Malongo??? Hujui mabaya aliyotenda pale ofisini kwako??? Hujui uzushi aliozushia watumishi pale huku akitamba wazi yuko karibu na Mh Magufuli?? Na akisema yeye ni seniour. yeye ni mmoja tu wa watesi wengi waliotesa watu ofisi ya VP yote inajua ubaya wa Malongo na genge lake alilojenga na bado yuko serikalini. Sio yeye tu na wengine wengi wapo na wameumiza sana watu..Kuna kesi zilifunguliwa za ajabu ajabu waliofanya hayo wapo serikalini..Mama hawa watakusumbua na wanataka ukwame ..fukuza hawa anza na watu wako...

LAKINI BADO yuko Serikalini...Ungeunda Serikali yako hawa watakuchanganyia madesa..fukuza hawa watu.
 
Back
Top Bottom