Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna viongozi wa mikoa na wilaya wanaendeleza matumizi mabaya ya madaraka hasa eneo la ukamataji.
Rais Samia amesema hayo wakati akitoa hotuba baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Kamati ya Haki Jinai iliyotolewa na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Ombeni Sefue Juni 15, 2024 Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
Akitoa hotuba yake kuhusu suala la matumizi mabaya ya madaraka Rais Samia anasema:
Matumizi mabaya ya madaraka ambayo linatakiwa kuwa jambo la kihistoria. Waraka namba 1 wa mwaka 2023 wa Katibu Mkuu Kiongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa wilaya unaoelekeza na kusisitiza uzingatiaji wa sheria na kanuni katika utekelezaji wa mamlaka yao ya ukamataji uende ukatekelezwe vyema.
Pamoja na waraka ule ambao umetolewa mapema mwaka jana bado kuna Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaendeleza ubabe wa maeneo walipo. Na nikimnukuu Makamu Mwenyekiti wakati ananipa breafing anasema wakati wa kikao chao na Wakuu wa Wilaya mmoja alisema mimi ni Mwakilishi wa Rais hapa kwahiyo lolote lililopo huku ni la kwangu, hata nikihisi mahakama imeamua sivyo mimi nitatengua. Sasa nadhani bado hatujakaa vizuri, aidha elimu zaidi inahitajika au kuna usugu fulani ambao unahitaji kushughulikiwa.
Kwahiyo niseme kwamba waraka ule uzingatiwe na uende ukafanye kazi vizuri, lazima kila mmoja kati yetu uwe Serikali Kuu au Serikali za Mitaa tujue taratibu za kazi zetu na mipaka yetu. Kila nafasi ina mipaka yake. Kwahiyo twendeni kwa mipaka yetu.
PIA SOMA- Mkuu wa Mkoa Chalamila: Nimeacha ubabe