Rais Samia: Bado kuna Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanatumia vibaya madaraka yao

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna viongozi wa mikoa na wilaya wanaendeleza matumizi mabaya ya madaraka hasa eneo la ukamataji.

Rais Samia amesema hayo wakati akitoa hotuba baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Kamati ya Haki Jinai iliyotolewa na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Ombeni Sefue Juni 15, 2024 Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Akitoa hotuba yake kuhusu suala la matumizi mabaya ya madaraka Rais Samia anasema:

Matumizi mabaya ya madaraka ambayo linatakiwa kuwa jambo la kihistoria. Waraka namba 1 wa mwaka 2023 wa Katibu Mkuu Kiongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa wilaya unaoelekeza na kusisitiza uzingatiaji wa sheria na kanuni katika utekelezaji wa mamlaka yao ya ukamataji uende ukatekelezwe vyema.
Pamoja na waraka ule ambao umetolewa mapema mwaka jana bado kuna Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaendeleza ubabe wa maeneo walipo. Na nikimnukuu Makamu Mwenyekiti wakati ananipa breafing anasema wakati wa kikao chao na Wakuu wa Wilaya mmoja alisema mimi ni Mwakilishi wa Rais hapa kwahiyo lolote lililopo huku ni la kwangu, hata nikihisi mahakama imeamua sivyo mimi nitatengua. Sasa nadhani bado hatujakaa vizuri, aidha elimu zaidi inahitajika au kuna usugu fulani ambao unahitaji kushughulikiwa.
Kwahiyo niseme kwamba waraka ule uzingatiwe na uende ukafanye kazi vizuri, lazima kila mmoja kati yetu uwe Serikali Kuu au Serikali za Mitaa tujue taratibu za kazi zetu na mipaka yetu. Kila nafasi ina mipaka yake. Kwahiyo twendeni kwa mipaka yetu.
PIA SOMA
- Mkuu wa Mkoa Chalamila: Nimeacha ubabe
 
Yaani Samia sijui kuna nini kinampa kigugumizi kwenye katiba mpya. Angelisimamia hilo kikamilifu, mapungufu yake madogo madogo tungeyasamehe, maana kwenye mambo ya haki, kajitahidi sana. Amejitahidi sana kupunguza ubabe wa viongozi na Polisi.

Rais Samia, shughulikia suala la katiba ushuhudie hata wakosoaji wako wakuu watakavyokuunga mkono.

Marekani wana Baba wa Taifa na pua wana baba wa demokrasia. Sisi tuna Baba wa Taifa, lakini Baba/Mama wa demomrasia hatujampata. Ina maana Rais Samia hataki kuochukua hiyo nafasi ili jina lake lidumu milele kwenye kumbukumbu?
 
Kuna video niliona YouTube viongozi wakikamata madada poa sinza, hiyo ni sawa kabisa na nawapongeza viongozi sababu ukahaba ni jinai na unaongeza maambukizi ya ukimwi shida yangu mimi kuna dada na bwana wake nao walikamatwa na kuoneshwa sura zao, japo mdada alijitetea kwa nguvu akisema niko hapa guest na mtu wangu, na viongozi hawakujali, binafsi sikufurahia kabisa wapenzi wale wawili kukamatwa haikuwa sahihi na ilinichukiza sana uhuru wao wa faragha ukivunjwa, you can only see this in Africa!!

Mama please sema na hao viongozi wanaokamata kamata raia na kuvunja uhuru na heshma za raia.
 
Naunga mkono hoja,hili lakatiba, Maza tumemshauri sana tuu
  1. Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
  2. Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
  3. Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
  4. Ombi kwa Rais Samia: Japo wengi wape, wachache pia wasikilizwe, Hoja ya kufanya minimum reforms za Katiba ni hoja ya msingi sana kuliko hata Sheria!.
P
 
Safi sana mama,hakika unawajibika,sasa hivi mambo ya kujitutumua kwa wakuu wa mikoa na wilaya naona yamepungua kwa 99.9%.

Mimi ni muumini wa utawala wa sheria naona hata mama naye ni muumini mkubwa wa jambo hili,tulifikia kipindi mkuu wa wilaya/Mkoa angeweza kuondoka na mkeo bila mwenye mke kuhoji.

Asante sana mama kwa uwezo wako wa kukemea,samia for 2025-2035,sio mitano tena kwa sasa,ni mikumi kabisa
 
Yaani Samia sijui kuna nini kinampa kigugumizi kwenye katiba mpya. Angelisimamia hilo kikamilifu, mapungufu yake madogo madogo tungeyasamehe, maana kwenye mambo ya haki, kajitahidi sana. Amejitahidi sana kupunguza ubabe wa viongozi na Polisi.

Rais Samia, shughulikia suala la katiba ushuhudie hata wakosoaji wako wakuu watakavyokuunga mkono.

Marekani wana Baba wa Taifa na pua wana baba wa demokrasia. Sisi tuna Baba wa Taifa, lakini Baba/Mama wa demomrasia hatujampata. Ina maana Rais Samia hataki kuochukua hiyo nafasi ili jina lake lidumu milele kwenye kumbukumbu?
Wahafidhima ndani ya chama ndiyo tatizo. Hao muda wote wanalinda maslahi ya ccm tu. Na siyo maslahi ya nchi.
 
Kuna video niliona YouTube viongozi wakikamata madada poa sinza, hiyo ni sawa kabisa na nawapongeza viongozi sababu ukahaba ni jinai na unaongeza maambukizi ya ukimwi shida yangu mimi kuna dada na bwana wake nao walikamatwa na kuoneshwa sura zao, japo mdada alijitetea kwa nguvu akisema niko hapa guest na mtu wangu, na viongozi hawakujali, binafsi sikufurahia kabisa wapenzi wale wawili kukamatwa haikuwa sahihi na ilinichukiza sana uhuru wao wa faragha ukivunjwa, you can only see this in Africa!!

Mama please sema na hao viongozi wanaokamata kamata raia na kuvunja uhuru na heshma za raia.
kale ka pimbi ka DC ka Ubungo anaitwa Hasani. kajaa kashamba sana na kajinga. nimeona kuna mtu kamchana kwenye akaunti yake ya Instagram juu ya operesheni yake ya kifala
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna viongozi wa mikoa na wilaya wanaendeleza matumizi mabaya ya madaraka hasa eneo la ukamataji.

Rais Samia amesema hayo wakati akitoa hotuba baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Kamati ya Haki Jinai iliyotolewa na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Ombeni Sefue Juni 15, 2024 Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Akitoa hotuba yake kuhusu suala la matumizi mabaya ya madaraka Rais Samia anasema:

Matumizi mabaya ya madaraka ambayo linatakiwa kuwa jambo la kihistoria. Waraka namba 1 wa mwaka 2023 wa Katibu Mkuu Kiongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa wilaya unaoelekeza na kusisitiza uzingatiaji wa sheria na kanuni katika utekelezaji wa mamlaka yao ya ukamataji uende ukatekelezwe vyema.
Pamoja na waraka ule ambao umetolewa mapema mwaka jana bado kuna Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaendeleza ubabe wa maeneo walipo. Na nikimnukuu Makamu Mwenyekiti wakati ananipa breafing anasema wakati wa kikao chao na Wakuu wa Wilaya mmoja alisema mimi ni Mwakilishi wa Rais hapa kwahiyo lolote lililopo huku ni la kwangu, hata nikihisi mahakama imeamua sivyo mimi nitatengua. Sasa nadhani bado hatujakaa vizuri, aidha elimu zaidi inahitajika au kuna usugu fulani ambao unahitaji kushughulikiwa.
Kwahiyo niseme kwamba waraka ule uzingatiwe na uende ukafanye kazi vizuri, lazima kila mmoja kati yetu uwe Serikali Kuu au Serikali za Mitaa tujue taratibu za kazi zetu na mipaka yetu. Kila nafasi ina mipaka yake. Kwahiyo twendeni kwa mipaka yetin
Anaonekana kulalamika tu kama sisi wananchi tunavyolalamika matarajio nikuchukua hatua wanaoenda kinyume na utaratibu na sivinginevyo
 
Kuna video niliona YouTube viongozi wakikamata madada poa sinza, hiyo ni sawa kabisa na nawapongeza viongozi sababu ukahaba ni jinai na unaongeza maambukizi ya ukimwi shida yangu mimi kuna dada na bwana wake nao walikamatwa na kuoneshwa sura zao, japo mdada alijitetea kwa nguvu akisema niko hapa guest na mtu wangu, na viongozi hawakujali, binafsi sikufurahia kabisa wapenzi wale wawili kukamatwa haikuwa sahihi na ilinichukiza sana uhuru wao wa faragha ukivunjwa, you can only see this in Africa!!

Mama please sema na hao viongozi wanaokamata kamata raia na kuvunja uhuru na heshma za raia.
Umewahi kufuatilia hiyo biashara
 
Kuhangaika na madada POA ni ujinga na upumbavu mkubwa sana! Kamata mafisadi wanaofilisi nchi yetu acheni upumbavu wenu!
 
Yaani Samia sijui kuna nini kinampa kigugumizi kwenye katiba mpya. Angelisimamia hilo kikamilifu, mapungufu yake madogo madogo tungeyasamehe, maana kwenye mambo ya haki, kajitahidi sana. Amejitahidi sana kupunguza ubabe wa viongozi na Polisi.

Rais Samia, shughulikia suala la katiba ushuhudie hata wakosoaji wako wakuu watakavyokuunga mkono.

Marekani wana Baba wa Taifa na pua wana baba wa demokrasia. Sisi tuna Baba wa Taifa, lakini Baba/Mama wa demomrasia hatujampata. Ina maana Rais Samia hataki kuochukua hiyo nafasi ili jina lake lidumu milele kwenye kumbukumbu?
Katiba hawezi kugusa ni mali ya CCM, na CCM wanafahamu ujanja ujanja unaowaweka madarakani ni kwa kutummia mapungufu ya katiba tuliyonayo. Kushughulika na hilo ni kukizika chama chao.

Wote wanafahamu hilo na hawalikubali kamwe.
 
Back
Top Bottom