Rais Samia: Barabara ya Tabora - Mpanda unateleza na lami tu

Rais Samia: Barabara ya Tabora - Mpanda unateleza na lami tu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.24_77852514.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Katavi ambapo sasa barabara ya kutoka Tabora hadi Mpanda (km 352) ni ya kiwango cha lami.

Rais Dkt. Samia ameeleza hayo leo Julai 13, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Inyonga Wilayani Mlele wakati wa ziara yake mkoani Katavi.

“Wakati nimekuja kipindi cha kampeni kutoka Tabora kwenda Mpanda ilikuwa ni vumbi tupu lakini leo nimeteleza mpaka nimesinzia, Barabara ni nzuri na ni maendeleo makubwa sana, Niwapongeze sana”, amesema Dkt. Samia.

Dkt. Samia ameeleza miradi mingine inayoendelea kutekelezwa na Serikali katika Mkoa wa Katavi ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Kibaoni - Makutano ya Mlele (km 50), Vikonge - Luhafwe (km 25), Luhafwe - Mishamo (km 37) na Kagwira - Karema (km 110) kwa kiwango cha lami.
WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.25_d8440454.jpg

WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.26_7306c1d9.jpg
Aidha, Dkt. Samia ameeleza kuwa pamoja na miradi inayoendelea kutekelezwa, Serikali ipo katika hatua za kutafuta Makandarasi wa kutekeleza miradi mingine ya miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Katavi.

Ametoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Katavi kutunza na kulinda miundombunu ya Barabara iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa.
 
Bara bara nyingi nzuri Tanzania zinatumiwa na magari ya Transit yanayotoka Bandarini kuelekea Nchi jirani huku Wazawa wakijibana kwenye Kimbinyiko na Vipasso au Prado mchagaa inayochomoka matairi ya mbele kwa sababu ya kodi kubwa ya kuingiza magari isiyolipika ya TRA...
 
Back
Top Bottom