Rais Samia: Bei ya Mafuta nchini ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine, Wananchi muwe watulivu

Rais Samia: Bei ya Mafuta nchini ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine, Wananchi muwe watulivu

Yaani shilingi 3800+ mpaka 4000+ kwa Lita 1 ni hela ndogo kwa Mtanzania! Halafu ishu ya bei ya mafuta kwenye nchi yako unailinganisha vipi na ile ya nchi nyingine? Tunalingana na hizo nchi kimaisha na kipato cha mwananchi mmoja mmoja?

Hivi hii nchi tumelaaniwa na nani mpaka tukapewa viongozi wa aina hii!!!
Anasahau kuna kitu kinaitwa purchasing power ya mtanzania ni tofauti kabisa na hizo nchi za ulaya.
 
Yaani shilingi 3800+ mpaka 4000+ kwa Lita 1 ni hela ndogo kwa Mtanzania! Halafu ishu ya bei ya mafuta kwenye nchi yako unailinganisha vipi na ile ya nchi nyingine? Tunalingana na hizo nchi kimaisha na kipato cha mwananchi mmoja mmoja?

Hivi hii nchi tumelaaniwa na nani mpaka tukapewa viongozi wa aina hii!!!

Marekani lita moja ni usd 8000, sasa fanya 2600x8000 😄 kweli wako juu
 
Analinganisha na Marekani labda mamaduro
Hata Marekani mafuta sio expensive kama anavyodai Bi Chura
Screenshot_20260408-155819.png
 
Rais Samia amedai kuwa bei ya Mafuta nchini ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine licha ya kupunguza ushuru, wananchi muwe watulivu hili jambo halijasababishwa na Serikali yetu.

Katika hotuba hiyo, Samia alinukuliwa akisema bei ya lita moja ya mafuta barani Ulaya imefika Euro 6,000 (takriban Tsh. Milioni 18), kabla ya kufanya marekebisho ya papo hapo kuwa ni kati ya Dola 500 na 800—kiwango ambacho bado kimezua taharuki kwa kuwa ni kikubwa mno kulinganisha na hali halisi ya soko la dunia.
 
Kwanini Samia hajawai kudimama upande wa wananchi kwenye matatizo kama haya mara nyingi uwa anakuja kutetea na kukandamiza
Kwa sababu hawawajibiki kwa hao wananchi, anawajibika kwa hao waliomweka na kumlinda abaki madarakani.

Hana sababu yoyote ya kuwa upande wa wananchi, kwa sababu hakutegemea kura zao kumweka madarakani.
 
Back
Top Bottom