Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Rais Samia Suluhu Hassan, akiweka Jiwe la Msingi Makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi leo Mei 28, 2025 Jijini Dodoma amesema;
"Tukio hili la kuweka jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi lina umuhimu wa pekee kwa upande mmoja linaakisi ndoto ya waasisi wa Chama chetu wakiongozwa na Mwenyekiti wetu wa kwanza wa Chama hiki Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kwa upande mwingine tukio hili linathibitisha umadhubuti wa Chama chetu na uwezo wake wa kupanga, kuamua na kutenda mambo makubwa na yenye maslahi kwa chama na Taifa letu.Ninaamini kuwa baada ya kukamilika kwa jengo hili sio tu tutalitumia au litatumika kwa kazi za utawala, bali pia itakuwa ni alama nyingine isiyofutika ya uimara, umoja na utambulisho wa Chama Cha Mapinduzi ndani na nje ya nchi.
Tutakuwa na jengo la kisasa linaloakisi sio tu ukubwa wa Chama chetu bali pia nafasi ya Chama hiki kuiongoza nchi yetu Tanzania lakini pia kuwa Chama kikubwa ndani ya Afrika lakini hasa kusini mwa bara la Afrika."