Rais wetu na vyombo vya ulinzi na usalama nchini,
Salaàm!
Nimefuatilia mienendo ya kukijenga chama cha CDM hapa nchini - iko wazi kuwa CDM wanatumia njia hiyo kama sehemu ya haki yao ya kukusanyika, kuandamana, kuongea na kutoa maoni.
Kinachonipa mashaka ni iwapo wanatumia forum HIYO kistarabu
* Kashfa kwa baadhi ya viongozi waliofariki zimekuwa nyingi;
* Kashfa kwa viongozi walioko madarakani zimekuwa nyingi - hususan uzanzibari, kuondolewa kwa maasai ngorongoro, dp world nk
Maridhiano si matusi, dhihaka na kuzua uongo. CDM wasipodhibitiwa mapema hapo baadae watajenga usugu.