Rais Samia: Chalamila wewe ni mfanyakazi mzuri ila naomba ukakue

Rais Samia: Chalamila wewe ni mfanyakazi mzuri ila naomba ukakue

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Rais Samia amemwambia RC Chalamila kuwa yeye ni mfanyakazi mzuri sana ila ni mtundu mno.

Amesema alimuacha kipindi kilichopita ila anaamini sasa amekua, akili imekua anamuomba aende akakue, amesema asidhani kupata nafasi ndio kamaliza, anamfuatilia kwa karibu sana.
 
Rais Samia amemwambia RC Chalamila kuwa yeye ni mfanyakazi mzuri sana ila ni mtundu mno.

Amesema alimuacha kipindi kilochopita ila anaamini sasa amekua, akili imekua anamuomba aende akakue, amesema asidhani kupata nafasi ndio kamaliza, anamfuatilia kwa karibu sana.
Ina maana rais hakuwa na option nyingine mpaka amrudishe Chalamila?
 
Raisi yuko Sahihi Chalamila na Makongoro Nyerere wanatakiwa kujua vyeo vikubwa kama vya kuteuliwa viwe ukuu wa mkoa etc na Raisi they need to behave themselves as senior responsible government officials not as comedians Or playboys.Nafasi hizo ni kubwa
 
Rais Samia amemwambia RC Chalamila kuwa yeye ni mfanyakazi mzuri sana ila ni mtundu mno.

Amesema alimuacha kipindi kilochopita ila anaamini sasa amekua, akili imekua anamuomba aende akakue, amesema asidhani kupata nafasi ndio kamaliza, anamfuatilia kwa karibu sana.
Juzi tu kateuliwa akaanza kuimba Mapambio na Mkewe ya kusherekea .... sasa sijui kakua lini.....!!
 
Hili neno Naomba huenda linawapa kujisahau wajibu wao wa kazi..!
 
Raisi Kaonya

Makongoro Nyerere na Chalamila they treat so lightly cheo cha ukuu wa mkoa

Wanajigeuza comedians au playboys hawatambui kuwa wao ni senior Government officials wanaohitaji ku behave themselves!! As Senior Government officials

Anyway it is a last warning
Hao ndio wanafaa msituletee mijitu ikipata ukuu wa wilaya au mkoa inajiona kama untouchable , kama yale majambazi Sabaya na matako Bashite
 
Sijawahi ona mhemhe wa hovyo kama Chalamila aisee, si kwa kudhalilishwa huko tena na mwanamke ptuuuuh.... nimemdharau sana hasa kwa silka ya wanaume wa kihehe.
 
Kama hii ndio sababu ya kupewa ukuu wa Mkoa Chalamila basi tutegemee siku yoyote atatemeshwa, huwezi kubadilisha tabia ya mtu kisa umempa cheo.

Kwanini Rais asitafute wasio na huo upungufu maisha yanendelee? hakuna zaidi ya Chalamila? kwa hili namshangaa Rais, wala simshangai Chalamila.

Very funny!
 
Back
Top Bottom