Pre GE2025 Rais Samia: Cheo ni sawa na nguo ya kuazima ambayo siku yoyote mmiliki wa nguo anaweza kuichukua!

Pre GE2025 Rais Samia: Cheo ni sawa na nguo ya kuazima ambayo siku yoyote mmiliki wa nguo anaweza kuichukua!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816

Rais Samia amewaonywa Viongozi wote walio pewa dhamana kukumbuka kuwa cheo ni sawa na nguo ya kuazima hivyo wanapaswa kutenda kazi kwa uadilifu na kwa masilahi ya nchi, ameyasema hayo wakati akiwaapisha viongozi walio teuliwa hivi karibuni baada ya utenguzi.

Pia soma: Mpango: Kiongozi usifikiri nafasi yako haiwezi kuzibwa

Acheni kutanguliza matamanio yenu mkasahau wajibu wenu kama viongozi.

Amewaonya viongozi wote kujirekebisha kabla hajagundua nyenendo zao maana panga litawashukia bila kuwaangalia usoni.

Aidha, kwa upande wake Makamu wa Rais Dkt. Mpango amewatahadharisha viongozi wote kuwa; wasijidanganye kuwa nafasi zao haziwezi kuzibika na kujifanyie wanavyotaka wataadhirika.

Tupo pamoja na Rais wetu kwa kila jambo analolifanya kwa masilahi ya wananchi na Taifa letu.
Kazi iendelee
 
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan awaapisha viongozi wapya wateule leo July26,2024 ikulu Dar es salaamwakiwemo mawaziri wa habariteknolojia na mawasiliano, Jerry Silaa,waziri wa ardhi nyumba maendeleo na makazi Deo Ndejebi, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano Afrika mashariki balozi Mahmoud Thabit Kombo, na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu{kazi,vijana,ajira,na wenye ulemavu}Ridhiwani kikwete.
 
Kumbe ni kweli wale jamaa walikuwa wanaiba pesa za walipa kodi ili waweze kutimiza malengo yao kisiasa.

Sasa kama ni wezi kwanini yule mmoja alimhamisha wizara aliyokuwepo akampeleka nje? alitakiwa kumtumbua pale pale.

Na kuwatumbua tu haitoshi, anatakiwa kuhakikisha wanafikishwa mahakamani wakajibu tuhuma dhidi yao za wizi na rushwa.
 
Shida ni kua mnatumbuana tu halafu inakua imeishia hapo.
Kama aliiba hata hicho alichokiiba anabaki nacho.

Hii sasa itafanya wale walioingia kwa dhamira za kuiba mali za umma wahakikishe wanaiba kwa kasi na kiasi kikubwa kadiri wanavyoweza ili ikitokea wametumbuliwa basi wawe na faida nzuri tu.

Ingekua ikigundulika umeiba basi sheria ichukue mkondo wake, waadhibiwe kwa mujibu wa sheria na sio kwa mujibu wa mteuzi.
 
Uchaguzi ujao tukawakate majina yao wezi wote... wakitaka wakagombee upinzani ili rangi zao tuzione vyema
 
Rais Samia amewataka Mawaziri wote kuheshimu viapo vyao kwani Kiapo kinapiga

Rais Samia amesema " Kiapo kinapiga Ukikiendea upande hakitakuacha Kitakupiga na Ukikidhihaki hakitakuacha Kitakupiga '

Source: Swahili Times

Jumaa Mubarak 😃
Mbona hakimpigi bashe na Mwigulu!
 
Back
Top Bottom