a hivi Tanzania kuna ugonjwa tumeupatawa wa kufikiri na kuamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ni cha kweli, nimesoma baadhi ya mambo wengine wanasema serikali imeiba Sh. Trilioni 1.5, nikamuuliza CAG mbona kwenye ripoti yako uliyonisomea hapa Ikulu hukunieleza huu wizi? Hii trilioni 1.5 mbona hamna, sasa hawa wa trilioni 1. 5 uliwaficha wapi? CAG Prof. Assad akanijibu hakuna kitu kana hicho, Katibu Mkuu akasema hakuna hakuna trilioni 1.5 iliyoibiwa na serikali.
“Sababu ya uhuru wa mtu kuandika chochote, nikacheka tu, hata ndege tuliambiwa ni mbovu, mtu hamuogopi Mungu, anaandika na kuaminisha watu, ningempata hata kama angekuwa Waziri siku hiyo hiyo angeondoka, natafuta hela halafu ziwe zinaibiwa. Lakini kwa vile ipoti ya CAG huwa inajadiliwa kwenye PAC, Wabunge watajadili wataona.
“Unapotosha umma wa Wa-Tanzania milioni 55, madhara yake ni makubwa sana, lazima tutangulize maslahi ya nchi yetu mbele, inawezekana kuna watu wanakuchukia wewe Jaji Mkuu ama wananichukia mimi, chuki hii tusiipeleke kwa Watanzania, naamini katika sheria hizi, kesi kama hizi zikija mtazishughulikia haraka haraka.
“Tanzania tunaipenda sote, nchi hii ikiharibika hayupo atakayebaki salama, tunaweza tukafikiri tupo pembeni, lakini madhara yake ni makubwa kwelikweli,”